A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 20, 2018

Yanga SC kurejea leo usiku


Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga wanatarajia kurejea majira ya saa 7:10 usiku wa leo kutoka Ethiopia walipokuwa wakicheza mchezo wao wa klabu bingwa Barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha.

Kabla ya kurejea nchini kikosi cha Yanga SC kimepata nafasi ya kula chakula cha mchana nyumbani kwa balozi wa Tanzania jijini Addis Ababa.

Yanga SC inarejea nyumbani ikiwa na furaha ya kufanikiwa kusonga mbele hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuisukumiza nje timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia kwa jumla mabao 2 – 1.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages