A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, April 3, 2018

Wema Sepetu afunguka kuna kundi la watu linamfanyia fitna


Baada ya malkia wa filamu Wema Sepetu kuchukua tuzo mbili za SZIFF 2018, amefunguka kwa kudai kuwa kuna kundi la watu linamfanyia fitna aonekane hakuna anachokifanya katika tasnia ya filamu.

Baada ya malkia wa filamu Wema Sepetu kuchukua tuzo mbili za SZIFF 2018, amefunguka kwa kudai kuwa kuna kundi la watu linamfanyia fitna aonekane hakuna anachokifanya katika tasnia ya filamu.

Muigizaji huyo ameyasema hayo leo hii wakati akiwashukuru wadau mbalimbali waliofanyika kuchukua tuzo hizo mbili. Kupitia Instagma Wema ameandika.

Napenda kuchukua nafasi hii Kumshukuru kwanza Allah Sub’hannah wata’Allah kwa kunifkisha hapa nilipo sasa… Najua ni mambo mengi sana yanafanyika kwa ubaya juu yangu ila yeye ndo amekuwa Tumaini langu kubwa… Nimshukuru Mama angu mzazi pamoja na familia yangu yote kwa ujumla kwa kusimama na mimi bega kwa bega katika kila kitu.

Nitoe n shukran zangu za dhati kabisa kwa Azam Tv kwa kutupa wasanii wote wa Tasnia ya Filamu fursa hii kubwa ya kuweza kujua nani zaidi… Hakika ni Changamoto nzuri sana na naiona inakuja kuleta mabadiliko makubwa kwenye Tasnia yetu.

Napenda kutoa Special thanks to my Love, The Woman behind The Best Actress 2018, My Tyler Perry, wanamuita Neema Ndepanya kwa kuniamini na kuniongoza vyema katika kazi… Najua upo very proud na nakuahidi kuendelea kuku make proud… We have so much to do mamy… @neema_ndepanya
Wema Sepetu Empire, Nawapenda sana watoto wangu… Nyinyi ni zaidi ya Ndugu sasa… Na tunaenda kufanya mapinduzi makubwa sana .. Maana sio kwa hasira nilizonazo sasahivi… .

Last But Not Least…. Wema Lovers… Hizi tuzo ni zenu… Nawashukuru kwa kunipa endless support kila ninapohitaji… Bila nyinyi siwezi… Ntaendelea kuwapenda na kuwathamini mpaka siku nakata kauli… .

Pia nichukue nafasi hii kuwashkuru wasanii wenzangu wote tulioshiriki kwenye tuzo hizi na kuwapa hongera maana hata kuwa nominated tu ni hatua kubwa sana… .

Mwisho kabisa nawashkuru wasanii WOTE wa Tasnia ya Filamu kwa ujumla… Tutakutana mwakani tena kwenye TUZO… Inshallah…

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages