A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 19, 2018

Tambwe afunguka anaumizwa na hali aliyokuwa nayo


Mchezaji wa klabu ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga Amisi Tambwe amefunguka na kudai anaumizwa na hali aliyokuwa nayo kwa sasa ambayo inampelekea kutokuonekana dimbani akiwa analisakata kabumbu huku akiwapongeza wachezaji wenzake kwa hatua nzuri waliyofikia katika mashindano.

Tambwe amebainisha hayo mchana wa leo Aprili 19, 2018 kupitia ukurasa maalum wa klabu yake baada ya kuadimika kwa kipindi kirefu kutoonekana uwanjani kutokana na majeruhi aliyokuwa nayo kwa sasa.

"Nawapongeza wachezaji wenzagu kwa kufanikiwa kuingia kwenye hatua ya makundi, nawashukuru wanayanga kwa jinsi wanavyonisapoti wakati huu wa majeraha yangu, naumia sana kutokucheza lakini hili ndiyo soka", amesema Amis Tambwe.

Timu ya Yanga imefanikiwa kuingia hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1, licha ya kufungwa katika mchezo wao wa marudiano na wapinzani wao Welayta Dicha. Leo wanatarajia kurejea nchini majira ya saa 1:00 usiku wakiwa wanatokea nchini Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages