Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai kuna baadhi ya wananchi hususani wanaoishi mijini hawana desturi ya kuhifadhi chakula cha akiba majumbani mwao jambo ambalo ni baya linaweza kuhatarisha maisha yao kwani hata panya na mchwa huwa wanahifadhi
Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo Aprili 21, 2018 wakati alipokuwa anatoa salamu za kwa wananchi wa mkoa wa Dodoma waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi maghala na vihenge vya kisasa kwa ajili ya kuhifadhia chakula lenye uwezo wa kubeba tani elfu 20.
"Binadamu asiyekuwa na akiba ya chakula atakuwa waajabu sana, kama mchwa na panya wanaweka akiba ya vyakula je itakuja kuwa binadamu ?. Sisi watu wa mijini tukikaguliwa nyumba zetu hata debe ndani la mahindi hukuti wala nusu debe ya maharage kazi ni kwenda sokoni kila siku", amesema Ndugai.
Kwa upande mwingine, Spika wa Bunge Job Ndugai amempongeza Rais wa awamu ya tano Dkt. John Magufuli pamoja na wasaidizi wake akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kuweza kutekeleza ahadi zilizopo kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM).
No comments:
Post a Comment