Bao pekee la Erasto Nyoni limeipa Simba ushindi dhidi ya watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo.
Nyoni alifunga bao hilo katika dakika ya 37 kwa kichwa, kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa kushoto mwa Uwanja na mshambuliaji Shiza Kichuya.
Katika mchezo huo mashabiki wa Simba wlaijitokeza kwa wingi zaidi ya wale wa Yanga huku wakijitoa kuishangalia zaidi timu yao wakati wote.
Dakika 90 za mchezo mzima zimemalizika kwa Yanga kushindwa kupata kona hata moja wakati huo Simba wakipata kona 8.
Beki Hassan Kessy alitolewa nje mnamo kipindi cha pili kwa kadi ya pili ya njano na nyekundu kutokana na kitendo cha kumchezea faulo, Asante Kwasi.
Matokeo hayo yanaifanya Simba izidi kujiweka kileleni kwa kufikisha jumla ya alama 62 huku Yanga ikisalia na 48.aa
No comments:
Post a Comment