A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 13, 2018

Simba mwendo mdundo, yaichapa Mbeya City


Vinara wa mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC wameendeleza ubabe wao leo kwa mara nyingine tena kwa kumchapa mpinzani wake kwa mabao 3-1 mchezo wa raundi 25 ulichozwa katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo ya Simba yamepatikana katika nyakati tofauti tofauti ndani ya kipindi cha kwanza ambapo bao la kwanza lilipachikwa na Emmanuel Okwi mnamo mwa dakika 16 za mchezo huo na ilipofika dakika 32 Asante Kwasi aliiongezea timu yake bao la pili, huku vuta ni kuvute ikawa kubwa kwa Mbeya City na hatimaye naye ikafanikiwa kujipatia bao la kwanza mishare ya dakika 34 kupitia mchezaji wake Frank Hamisi, lakini kama hiyo haitoshi ilipofika dakika 35 nahodha John Bocco aliwasimisha mashabiki wa simba kwa kuwapatia bao la tatu.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza za mchezo huo kumalizika timu ya Simba SC ilikuwa mbele kwa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City.

Kipindi cha pili cha mchezo huo kilipoanza Mbeya City walionekana kubadilika kimchezo hali ambayo iliweza kuwapa matumaini mashabiki waliojitokeza kutazama mtanange huo lakini kwa bahati mbaya juhudi zao hazikuweza kuzaa matunda na kupelekea kuruhusu kuchambuliwa zaidi na wapinzani na mpaka kipenga cha mwisho kilipo pulizwa Simba walikuwa mbele kwa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City.

Kwa ushindi huo Simba SC imezidi kujikita kilele mwa msimamo wa ligi kuu kwa alama 55 huku nafasi ya pili ikiendelea kushikiliwa na Yanga kwa alama 47, Azam FC kushika nafasi ya tatu kwa alama 45 huku nafasi ya nne ikiwa imekamatwa na Tanzania Prisons kwa alama 38.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages