A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 20, 2018

RC MAKONDA: WANAUME AMBAO HAMTAKI KUHESHIMU HAKI ZA WATOTO WENU NITAWAWAJIBISHA KWA MUJIBU WA SHERIA


Rc Makonda akizungumza na wanawake waliotelekezwa waliofika kupata msaada wa kisheria, ambapo amesema zoezi litaendelea kwa takribani siku tano ili.kushughulikia kesi zilizopokelewa.

Baadhi ya kina mama waliofika kupata msaada wa kisheria.


Mkuu wa mkoa.wa Dar es salaam Mhe.Paul Makonda amewataka wakina baba wote waliotumiwa wito wa kufika ofisini kwake kutokana na kulalamikiwa kutelekeza watoto kufika kwani watakaokaidi kwanzia jumatatu ya wiki ijayo watakamatwa na Polisi.

Rc Makonda ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wanawake waliotelekezwa waliofika kupata msaada wa kisheria kwa ajili ya haki za watoto wao,  amesema wakina baba wote waliopelekea wito na wakakaidi kufika na wengine kutukana ama kujibu kejeli kwanzia jumatatu ya wiki ijayo watakamatwa.

"Mwanaume yeyote ambaye amepigiwa simu ambaye amepelekewa barua  alafu amekaidi wito kwanzia Jumatatu  ninawakamata wanaume waliokimbia majukumu yao" Amesema Makonda

Amewataka wanaume wote wanaofahamu wana watoto wahakikishe wanawajibika kwa mujibu wa sheria kwani sheria ya mwaka 2009 inamtambua mtoto na haki zake.

Amesema hawezi kuendelea kuongoza mkoa wenye ongezeko la watoto omba omba mitaani wakati wa baba zao.

"Siwezi kuendelea kuongoza mkoa wenye idadi ya ongezeko la watoto omba omba wakati baba zao wapo" Amesema

Amesema zaidi ya watu 17,000/wamefika ofisini kwake na wakina mama 7,000 elfu saba wamesekilizwa na kwamba zaidi ya wanaume 15,000 wamekubali kisheria kutoa matunzo ya watoto wao na wengine kuchukua vipimo vya DNA.

Ameongeza kuwa zoezi hili limekuwa nzito na kubwa kutokana na idadi kubwa ya wakina mama wanyonge kushindwa kupata huduma kikamilifu hivyo amewataka watu wa ustawi wa jamii kufanya kazi zao kwa uaminifu na kwamba baadhi yao wamekuwa wakifanya kazi hiyo vibaya na kusababisha wakina mama hawa kutopata haki zao za msingi.

Aidha amesema katika serikali hii ya awamu tano kila mmoja atatekeleza majukumu yake ipasavyo.

Pia amesema kuwa kutokana na zoezi hili kuwa zito na kubwa wataunda kamati ya wanasheria ikishirikiana na ustawi wa jamii itakayosaidia kubaini chanzo cha tatizo hilo  ili kusaidia kupunguza idadi ya wakina mama hao wanaoteseka kwa muda mrefu bila ya kupata msaada kwa watoto kupata haki yao.

Rc Makonda amesema kutokana na Idadi kubwa ya Wakina mama hao kujitokeza na kuhudumiwa kwa takribani siku kumi wataendelea kushughulikia kesi zilizopokelewa ambapo ameongeza siku nyingine tano ili kuwasaidia kina mama hao waliofika kupata msaada wa kisheria katika ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages