A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, April 6, 2018

Magufuli kuzindua ukuta ya mgodi ya madini ya Tanzanite leo

Rais John Magufuli wa Tanzania, leo anatarajiwa kuzindua ukuta ya mgodi ya madini ya Tanzanite,iliopo eneo la Mererani, kaskazini mwa nchini Tanzania


Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.


Awali, Mwezi Februari , wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.


Walisisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.



Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages