Aliyekuwa Rais wa Brazil Luis InĂ¡cio Lula da Silva amegoma kujisalimisha kwa polisi kama alivyotakiwa na mahakama ya nchi hiyo hii leo, ili aanze kutumikia hukumu yake.
Rais huyo ambaye alishtakiwa kwa makosa ya rushwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka 12, alikuwa nje kwa dhamana, na mahakama ilimtaka aende mwenyewe kwani sio busara kwenda kumkamata Rais Mstaafu.
Rais Da Silva amesema mahakama hiyo ina lengo la kumuharibia mipango yake ya kugombea urais hapo Oktoba mwaka huu, huku akiwa na matumaini makubwa ya kushinda uchaguzi kutokana na kutajwa kuwa kipenzi cha watu.
Mamia ya watu wamezunguka eneo la umoja wa wafanyakazi, ambalo lipo karibu na eneo analoishi kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment