A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 25, 2018

Polisi Tabora ya ua Jambazi mmoja


Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora SACP WILBROD MUTAFUNGWA, tukio hili limetokea tarehe 24.04.2018 saa 22:50hrs maeneo ya Malabi kata ya Ipuli  ambapo majambazi wawili wakiwa na silaha aina ya shortgun na panga walivamia na kuvunja nyumba ya mfanyabiashara JANIFIO MWAKABALULA na kabla majambazi hao hawajafanikiwa kufanya tukio hilo askari  Polisi walipata taarifa na kufika eneo la tukio na katika harakati za kutaka kuwakamata majambazi hao mmoja aliyekuwa na panga alitaka kumjeruhi askari ndipo askari alifyatua risasi na kumpata jambazi huyo maeneo ya shingoni na kufariki dunia wakati anakimbizwa hospitalini.

Jeshi la Poisi Mkoani hapa limeendelea na misako ya kumsaka jambazi aliyekimbia na washirika wake na  wamefanikiwa kuwatia mbaroni watu wawili ambao ni wakazi wa Tabora akiwemo mganga wa kienyeji ambaye huwapatia kinga majambazi ili wasikamatwe na vyombo vya dora majina ya watu hao yameifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages