Washambuliaji wa Yanga Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma wameondolewa katika sehemu ya kikosi kitakachowavaa Waleyta Dicha katika mechi ya kesho.
Wawili hao wameondolewa baada ya kutonesha sehemu walizoumia ambazo baada ya kupona walianza mazoezi.
Dicha tayari iko nchini kuivaa Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.
Wachezaji hao walijitonyesha katika mazoezi ya mwisho ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema wachezaji hao walipona majeraha yao kabla ya kuanza mazoezi hayo na kujitonyesha.
No comments:
Post a Comment