A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, April 21, 2018

Mzee Akilimali aibuka na kutoa kauli kwa Yanga


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameitaka klabu yake kufanya usajili ili kukiboresha kikosi hicho ambacho kina wachezaji kadhaa walio majeruhi.

Mzee Akilimali ameomba Yanga ifanye usajili huo katika nafasi tatu ili kuweza kukipa makali kiweze kurejea kama ilivyokuwa miaka miwili nyuma.

Mjumbe huyo amewataka Yanga kusajili beki mmoja ili asaidiane na Abdallah Shaibu 'Ninja', pia akiomba asajiliwe mchezaji namba 8 na 9.

Akilimali amefikia kutoa ushauri huo kutokana na namna mwenendo wa kikosi ulivyo hivi sasa ambapo imekuwa na wachezaji ambao ni majeruhi kama Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao hawajacheza kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages