MBUNGE wa Geita vijijini, Joseph Kasheku (CCM), ‘Musukuma’, ameitaka serikali iwarudishe kazini watumishi wote wenye elimu ya darasa la saba iliowafukuza kazini, la sivyo hata wabunge wenye darasa la saba nao waondolewe bungeni.
Musukuma amesema hayo bungeni Mjini Dodoma leo Ijumaa, Aprili 6, alipokuwa akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2018/19 huku akidai wabunge hao wakishaondolewa bungeni warudishwe kwa Viti Maalumu kama ilivyo kwa wanawake na walemavu, ili wakawatetee wenye darasa la saba wenzao.
Aidha, Musukuma ameeleza kwamba, hotuba ya Waziri Mkuu inaonyesha mwaka wa fedha uliopita wanafunzi wa darasa la saba walikuwa milioni mbili lakini walijiunga na elimu ya Sekondari ni laki tano, na kudai kwamba inaonyesha wenye elimu ya darasa la saba ni wengi zaidi ya asilimi 80.
“Serikali isiposikia kilio chetu na kuwarudisha kazini watumishi wenye elimu ya darasa la saba, wabunge wote tuungane kutetea watumishi hao waliofukuzwa kazi,” alisema Musukuma.
No comments:
Post a Comment