A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 5, 2018

Mtanzania apandishwa kizimbani Uingereza akidaiwa kumuua mkewe

 RAIA wa Tanzania Kema Salum (38) amefikishwa mahakamani nchini Uingereza akidaiwa kumuua mkewe, Mtanzania pia, aitwaye Leyla Mtumwa.

Salum anayedaiwa kumchoma visu Leyla na kumuua wakiwa nyumbani kwao mtaa wa Kirkstall, Haringey, nchini humo Ijumaa iliyopita, amefikishwa katika mahakama ya Crown.

Kutokana na mgomo wa wanasheria nchini humo tangu kuanza kwa mwezi Aprili, kesi hiyo haikusikilizwa na Jaji Anuja Dhir ameahirisha usikilizwaji wake hadi Juni 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa mwanasheria Seona White, juhudi zinafanyika ili kupata wakili wa kumtetea Salum mahakamani licha ya mgomo wa mawakili unaoendelea.

Mtuhumiwa huyo alisomewa mashitaka yake kwa Kiingereza lakini kupitia mkalimani aliyemwelewesha kwa Kiswahili. Mipango inafanywa kumleta marehemu nchini Tanzania.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages