Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji wa Serikali Bw. Hassan Abbas, leo ametembelea Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Katika ziara yake hiyo, Bw. Abass aliipongeza Global Group kutokana na suala zima la habari kutokana na kuwa na watu wenye weledi wa hali ya juu, huku pia akipongeza namna kampuni hiyo inavyozalisha magazeti.
Bw. Abass amewataka waandishi wa habari kujiendeleza zaidi angalau kufikia levo ya diploma kwa wale ambao hawajafika levo hiyo kutokana na sheria waliyoiweka ambayo hapo baadaye wanahabari wote watatakiwa kuwa na angalau diploma ya uandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment