A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 5, 2018

Mrisho Mpoto: Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu?


Baada ya msanii Steve Nyerere kukosoa Tuzo za Filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF) kwa kueleza kuna baadhi ya wasanii walistahili kupata na hawakuapa, Mrisho Mpoto amemjibu kuhusu hilo.

Msanii huyo wa nyimbo za asili amemkosoa vikali Steve Nyerere kwa kueleza kuwa si mzalendo na kumtaka kupuguza Gubu kwa kumueleza kuwa Tuzo hizo zilitolewa kwa utaratibu uliyowazi kabisa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mpoto ameandika;

Steve Nyerere Mbona huna Jema ndugu? Uzalendo ni Hali ya Mtu kujitoa kufa na kupona Kwa maslahi ya wengi yenye Tija Kwa Taifa, nikakusikia kwenye vyombo vya habari unasema Uzalendo ni project yako, tena ukaenda Mbali zaidi ukasema nimedandia project yako kwa mbele, nikahisi tofauti kidogo: Kwakua kilikua kipindi cha jua kali kidogo.

Sasa hivi umeibuka na kuanza kuponda Tuzo za Sinema zetu ambazo ndiyo kwanza zinaanza ili kujaribu kurudisha Heshima ya filamu zetu ambazo wewe umechangia kufa kwake hauoni unakatisha tamaa watu wenye nia njema na Filamu? Ebu punguza gubu ndugu yangu angalau tuwe na kitu kimoja Chenye heshima cha kujivunia kwenye tasnia ya sanaa….ya uigizaji…

Zile Tuzo zilitolewa Kwa wenye Umiliki wa filamu na aliyewasilisha kwenye Mashindano na siyo anaeonekana sana kwenye Runinga…siyo lazima apewe unaemtaka wewe Stive. Najua kile kilikua kipindi cha jua, hiki cha mvua labda utanielewa kidogo…wadau na Mashabiki wa Bongo Movie msikatishwe tamaa.

Utakumbuka hapo jana Steve Nyerere alihoji ni kwanini Ray Kigosi, JB, Rich, Roams, Aunt Ezekiel, Shamsa Ford, Duma, Weru, Hemedi, Tausi Mndengela, Mainda, Johari, Uwoya, Marian Ismail na Batuli kutopatiwa tuzo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages