A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 26, 2018

MKOA WA DAR ES SALAAM WASHEREHEKEA SIKUKUU YA MUUNGANO KWA KUTOA MSAADA KWA WAHANGA WA MAFURIKO.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akipokea msaada wa vitu mbalimbali  kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Center Abdalah Seleman kwa niaba ya wanainchi waliokumbwa na mafuriko wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa taasisi hizo. hafla yamakabidhiano hayo yamefanyika leo jijini hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa Paul Makonda akizungumza jambo na viongozi wa Taasisi hizo kabla yakupokea msaada huo. hafla yamakabidhiano hayo yamefanyika leo jijini hapa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa Paul Makonda akitoa neno la shukurani mara baada yakupokea mdaada huo kwa niaba ya wanainchi waliokumbwa na mafuriko
Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Center Abdalah Seleman akizungumza katika hafla hiyo.

 Mkoa wa Dar es Salaam umeadhimisha sikukuu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 54 kwa kupokea Masada wa vyakula na magodoro kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko katika Mkoa huo. 

Akipokea misaada hiyo iliyotolewa na Taasisi mbili Za Miraj Islamic center na Abdullah Aid Uk Tanzania -Gamb Rc Makonda amsema ni faraja kubwa ambayo taasisi hizo wameonyesha umoja na mshikamano katika nchi yetu ambapo wamefanya jambo kubwa LA kuwakumbuka wahanga nao.

Amesema misaada hiyo ambayo ni Mchele, Vyandarua ,Magodoro,Mito, Unga,Pamoja na mafuta ambavyo  vitanufaisha zaidi ya familia 600 ambazo zilikumbwa na mafuriko hayo

Amesema mafuriko yapo ya aina mbili wapo wa mabondeni na wengine wale ambao nyumba zao zilifuatwa na maji na kusababisha kuishi kwa tabu kutokana na Mali pamoja na vyakula vyao kuachukuliwa na Maji. 

Aidha Makonda amesema ili waweze kugawanya misaada hiyo watamchukua Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ilala Ubaya Chuma kuratibu zoezi la Kagawa vyakula na malazi yanawafikia walengwa husika,kupitia wenyeviti wa Mitaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Miraji Islamic Center Abdalah Seleman amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kukubali kupokea Masada huo ili kuwasaidia wahanga wa mafuriko. 

Amesema taasisi hiyo inafanya kazi na taasisi mbalimbali pia ina anda vijana kwa kuwapatia elimu zote ili na wao waweze kuwa na Upendo na Moyo wa kutoa na kulitumia taifa hapo baadae.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Abdulah Aid UK Tanzania -Gambia Arif Ally Abdurahman amesema wameamua kuwakumbuka waathirika wa mafuriko kwani walikuwa wanaishi kwa tabu na shida.

Pia.wamempongeza Mhe.Rais John Magufuli kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu katika nchi na kuahidi kushirikiana na serikali katika kukuza maendeleo ya nchi.
















No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages