Halmashauri ya manispaa ya Ubungo imesema itaanza kutoa fedha kiasi cha bilioni moja nukta tisa(1.9) kwa ajili mikopo kwa kinamama, vijana na walemavu kuanzia mwezi Mei mwaka huu.Meya wa Ubungo, mheshimiwa Boniface Jacob leo Aprili 18,2018 akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB iliyoteuliwa na manispaa hiyo kwa ajili ya kutoa fedha hizo kwa wananchi, ameeleza kuwa, vijana na akina mama watapatiwa asilimia arobaini(40%) na walemavu asilimia ishirini(20%) ya fedha hiz“Watendaji hamasisheni vijana wajitokeze kuomba mikopo kwa sababu hadi sasa idadi ya waliojitokeza kuomba mikopo ni ndogo. Ubungo imetenga fedha nyingi za mkopo kuliko halmashauri yoyote nchini, imekuwa halmashauri ya kwanza kwa kufanya hivyo nchi nzima, hivyo wananchi wa Ubungo tumieni fursa hiyo,” amesema Meya Jacob.
Naye mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo, John Kayombo amesema hadi sasa vijana waliojitokeza kuomba mkopo ni 1124, huku kina mama 11312, wenye sifa na vigezo vya kupata mkopo wamejitokeza kuomba mkopo kutoka katika vikundi 970 vilivyosajiliwa na manispaa hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa idara ya watoa huduma wa kibenki mbadala kutoka CRDB, Phillip Alfred ameishukuru manispaa ya Ubungo kwa kuiteua benki hiyo kuwa rasmi katika kutoa huduma zake za kibenki.“Bodi ya CRDB inatoa shukrani kwa kuichagua kuwa benki rasmi ya kutoa huduma za kibenki kwa manispaa ya Ubungo. Tunaahidi kuwawezesha wanawake na vijana kupata mikopo ya riba nafuu kutoka CRDB,
“Tumetoa vigezo rahisi ili kuwezesha wanawake na vijana, kuanzisha miradi mbalimbali na kuwezesha uchumi wa mmoja mmoja ili kuona wanawake na vijana wanatoka kwenye hatua moja ya maendeleo kiuchumi kwenda nyingine, mikopo hii itarudishwa kwa wakati kadiri ya makubaliano ili kunufaisha wengine,” amesema Alfred.
No comments:
Post a Comment