Sherehe za maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yanafanyika katika Uwanja wa jamhuri mjini Dodoma ambapo Rais John Pombe Magufuli, ndiye mgeni rasmi.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa mnamo tarehe 26 Aprili, 1964 kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na walioziunganisha nchi hizi mbili ni baba wa taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume kwa kuchanganya udongo kutoka pande zote mbili za muungano.
No comments:
Post a Comment