MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James amesema haitatokea chama hicho kikatolewa madarakani katika chaguzi zozote huku akieleza Watanzania wa sasa wana akili sana katika kuamua mambo yao hasa yahusuyo uchaguzi.
“Kwa kipindi hiki ambacho watanzania wana akili timamu, sidhani kama CCM itaweza kuanguaka madarakani. Watanzania wana akili sana na wanaiona kesho kubwa ya nchi hii na usalama wa Tanzania bado upo CCM. Hatuzui wapinzani lakini kwa dola ni CCM tu, itaendelea kutawala sana,” amesema Kheri.
Aidha, Kheri amesema kumekuwepo na wanasiasa wengi wanaoingia kwenye siasa kwa kufuata mkumbo na kuacha misingi ya kisiasa ambayo ni kuzungumza kwa hoja zenye tija kwa jamii pamoja na maslahi kwa taifa.
No comments:
Post a Comment