MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Irene Paul amewakata vilimi mastaa wa Bongo kwa kuwaambia kuwa hakuna staa mkubwa Bongo kama Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Irene alisema mrembo huyo wa Uganda ni mfano wa kuigwa kwani anajua kutengeneza jina lake na ni mtafutaji wa kweli.
“Ni staa mkubwa, anajua kumaintain jina lake, simuoni staa wa kumshinda yeye Bongo,” alisema Irene.
Kauli hiyo iliungwa mkono na baadhi ya mashabiki waliomsikia muigizaji huyo alipokuwa kwenye utoaji wa tuzo za wasanii wa Kibongo ambazo ziliandaliwa na kituo cha Azam TV.
Stori: Mwandishi Wetu, Amani.
No comments:
Post a Comment