Mwanamuziki wa hip hop bongo mwenye sauti ya kipee Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amefunguka juu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kanisani, na kuwepo kwa tetesi za kuokoa.
Akizungumza na www.eatv.tv Chid Benz amesema kwamba alihudhuria kanisani hapo kwa sababu alialikwa, na sio kuokoka kama wengi wanavyodhani.
“Imani ni kitu fulani chepesi sana ingawa ni kigumu sana, mimi nilialikwa pale kama mgeni rasmi, kulikuwa kuna wabunge, wajumbe wa serikali, lakini mimi nilialikwa nisingeweza kukataa, tena nikaona ni bahati ni siku yangu ya kuzaliwa, nikaona kwa nini nisende nikasikiliza nikaungana nao, mimi ni Rashid Abdala Makwilo, sijachange wala sijaongea kwamba nimeokoka”, amesema Chid Benz
Chid ameendelea kwa kusema kwamba....”sina mpango huo wa kuokoka, naishi katika misingi ambayo nawezakufuata imani yoyote jinsi inayonituma na kuheshimu dini nyingine, sio vibaya”.
Licha ya kuhudhuria kanisani hivi karibuni Chid Benz alionekana akiwa jukwaani na wanamuziki wa nyimbo za Injili, akiwemo Bony Mwaitege.
No comments:
Post a Comment