NYOTA wa zamani wa Real Madrid na Hispania, Xabi Alonso amesema anaona Hispania ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu huko Urusi pia klabu zake zitatwaa mataji ya Uefa.
Alonso alisema timu ya Taifa ya Hispania ina nafasi kubwa kutwaa ubingwa wa dunia ikitokea Kundi B la michuano hiyo mbele ya mataifa ya Iran, Morocco na Ureno.
“Timu ya taifa ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia, pia Real Madrid ina nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hata Atletico inaweza kuchukua Europa,” alisema Alonso.
No comments:
Post a Comment