Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda akiongea baada ya Airtel kuibuka kinara katika kutoa hudumia kupitia mitandao ya kijamii, akishuhudia Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Bi Singano Mallya
Airtel Tanzania imetajwa kuwa moja ya makampuni bora ambayo yanajibu vizuri
maswali ya mashabiki na wateja wake katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2018.
Ripoti hii imetolewa na kampuni ya Socialbakers ambayo ni moja ya makampuni
yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali
yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya
kijamii.
Kwa mujibu wa Socialbakers, tathmini ya robo hii ya mwaka ilifanyika kuanzia
Januari 1, 2018 hadi Machi 31, 2018 na kuifanya Airtel Tanzania iibuke kidedea.
Kampuni hiyo ya Social bakers imekabidhi cheti kama ishara ya ushindi huu na
kuonesha kuwa Airtel iliweza kujibu vizuri maswali ya mashabiki wake na wateja
kupitia mtandao wa Face book kwa asilimia 98 na hivi kuyapiku makampuni mengine
yote ya simu Tanzania.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda alisema
wanajivunia kupata utambulizi huo na inaonesha jinsi gani wamekuwa wakijituma
kuhakikisha wateja wao wanapata majibu ya maswali yao kwa wakati kupitia
mitandao ya kijamii hususani Face book.
“Tunayo faraja kuweza kutambuliwa kwa namna hii na sisi tunalo jukumu la
kuendelea kuhakikisha wateja na mashabiki wetu wanapata majibu wanayohitaji kwa
wakati na mitandao ya kijamii imeturahisishia kazi hii hususani kupitia Face
book tumeweza kujibu maswali kwa haraka na kwa wateja wengi zaidi kwa wakati
mmoja,” alisema.
Mitandao ya kijamii kama Face book inatakiwa kutangazwa zaidi ili itumike
kwa wingi kwani itapunguza usumbufu wa wateja kusubiri majibu kwa muda mrefu
kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walilazimika kupiga simu Airtel. “Kwa kupitia
mitandao ya kijamii majibu yanatolewa hapo hapo na hili ndilo limetufanya
tutambuliwe kwani tumeweza kutumia njia hii kwa ufanisi mkubwa na tathmini ya
Socialbakers imeonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu tulijibu maswali
kwa asilimia 98 na hivi kuibuka kidedea,” aliongeza Ndunda
Kwa mujibu wa Socialbakers, utambulizi huu unatokana na namna kampuni
imeweza kujibu maswali ya watu kwa muda wa mwezi mitatu. Ili utambuliwe, lazima
kampuniipokee maswali 50 kutoka kwa mashabiki katika robo husika na maswali
hayo yaweze kujibiwa kwa zaidi ya asilimia 65.
Socialbakers ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini
kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja
wao katika mitandao ya kijamii hususani Face book, Twitter, Google+, LinkedIn
na YouTube ili kusaidia makampuni kujua mafanikio ya kampeni mbalimbali kupitia
mitandao hii.
No comments:
Post a Comment