A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, March 28, 2018

WAZIRI wa Viwanda na biashara Charles Mwijage kuzindua maonyesho ya Wabunifu na Wavumbuzi



WAZIRI wa Viwanda na biashara,Charles Mwijage anatarajia kuzindua maonesho ya wabunifu na wavumbuzi ikiwa ni kutoa fursa kwa vijana ya kuendeleza kazi zao na kukuza ubunifu /uvumbuzi.


Maonesho hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Viwanda na biashara na taasisi mbalimbali ambazo ni Brela, Sido, Tantrade, Cosota na Costech ili kufikia Tanzania ya Viwanda.


Akizungumza Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati wa Kamati ya maonesho hayo, Edward Kilaka amesema maonesho hayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini na kwamba yanatarajia kufanyika April 27 hadi 29/2018 katika viwanja vya mnazi mmoja.


Amesema katika maonesho hayo mshindi wa kwanza atapata shilingi milioni 20 na mshindi wa pili atapata shilingi milioni 10 ambapo mshindi au washindi watatu watapata shilingi milioni 5.


Amesema washindi wa tatu watapata nafasi ya kuunganishwa na wafanyabiashara, makampuni makubwa ili waweze kuingia nao mkataba na kukuza ubunifu na uvumbuzi wao.


Ameongeza kuwa watapata nafasi ya kutembelelea nchi zilizoendelea ili wajifunze na kuongeza ubunifu wao na washindi wa mkoa huo watapata fursa ya kuzunguka bila malipo kupitia huduma ya taxify mwaka mzima.



"Tutazunguka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma... Tutachuja wabunifu na wavumbuzi 50,"amesema.


Kwa upande wake Ofisa Habari Wizara ya Viwanda na biashara, Edward Nkomola amesema maonesho hayo yataongeza uzalishaji wa bidhaa na huduma viwandani.


"Maonesho haya yatahudhuriwa na waheshimiwa, mabalozi wa nchi zote nchini, wafanyabiashara wakubwa na wa kati, taasisi za serikali na wananchi wote, "amesema.


Amesema vijana wengi ni wabunifu lakini wanakosa fursa za kuendeleza ubunifu wao, kujulikana na kupata ajira.


Meneja uzalishaji wa Kampuni ya Taxify, Remmy Eseka amesema ubunifu ni moja ya kazi yao katika kutoa huduma zao katika miji takribani 25 na kwamba wapo tayari kushirikiana nao katika maonesho hayo.


Aidha, kauli mbiu katika maonesho hayo ni 'Ubunifu kwa maendeleo ya viwanda na Tanzania, "amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages