Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dk. Grace
Maghembe, (kushoto), akikabidhi vifaa tiba vya Mama mzazi kwaajili ya kujifungulia
(Delivery Packs) kwa Mganga Mkuu wa Meno, wilaya ya Ubungo Safaa Chunga, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa
wilaya hiyo, hafla yamakabidhiano hayo imefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Dk. Grace Maghembe, akizungumza na waandishi wa habari kabla
yakukabidhi vifaa hivyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar
es salaam Mhe. Paul Makonda leo ametoa zawadi ya vifaa tiba vya Mama mzazi
kwaajili ya kujifungulia (Delivery Packs) 200 vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi million 20 Kama zawadi yake ya sikukuu ya pasaka kwa kinamama watakaojifungua
kwenye msimu huu wa pasaka.
Gharama ya mfuko mmoja (package) ya Vifaa hivyo vya kisasa ni
Shilingi laki Moja ambapo ndani yake kuna Mashuka, Vitambaa, Dawa, Mabomba ya
Sindano, Pamba, Kibanio cha kitovu, Nyuzi, pedi za kinamama, Dawa ya kuzuia upotevu
wa damu, Nyembe na Gloves ambapo vitatolewa Bure kwa Mama mzazi atakaejifungua
msimu huu wa pasaka kwenye vituo vya Afya na zahanati zilizopo kwenye Wilaya
Tano za Mkoa huo.
RC Makonda ametoa
vifaa hivyo baada ya kubaini changamoto ya baadhi ya kinamama kushindwa kumudu
gharama ya vifaa vya kujifungulia na kujikuta wanatumia kanga au nguo jambo
ambalo ni hatari kiafya kwa mama na mtoto.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya RC Makonda kwa waganga wakuu
wa halmashauri na wasimamizi wa vituo na Zahanati, Mganga mkuu wa mkoa wa Dar
es salaam Dr. Grace Maghembe amesema vifaa hivyo vitasaidia pia kupunguza vifo
vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Vifaa hivi vinapatikana Bure kwenye Hospitali zote za Mkoa wa
Dar es Salaam kwa Msimu huu wa Pasaka hivyo kwa wewe Mama unaetaka kujifungua
fika Hospitalini vifaa vyako utavikuta.
KUTOA NI MOYO, SIO UTAJIRI.
No comments:
Post a Comment