OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kitengo cha ardhi , imemtaka Msajiri wa Hati wa Wizara ya Ardhu,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufuta mara moja hati namba 105525 wa Kiwanja namba 1003 kilichopo Mtaa wa Sekenke Kinondoni, chenye mgogoro uliodumu kwa miaka 10.
Kiwanja hicho kilikuwa kinagombewa na wananchi wawili ambao ni Ally Abdi na Seleman Marashed kutokana na familia kukiuza mara mbili huku pia kikiwa na namba mbili ambazo ni 212 na 1003.Ofisi hiyo imebaini kunaupindishaji mkubwa wa taratibu za uuzwaji na upimaji wa kiwanja hicho ambacho kilikuwa ni mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Kwa mujibu wa barua ya Ofisi ya mkuu wa mkoa kwenda Wizara ya Ardhi, iliyosainiwa na Ofisa Ardhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Edgar Msolla, ya Februari 15 mwaka huu, baada ya uchunguzi mzito kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni ilibaini kuwepo ukiukwaji wa sheria.Uchunguzi huo umekuja baada ya Abdi kuwasilisha malalamiko katika ofisi hiyo kuhusu kiwanja hicho namba 212 ambacho kipo kwenye mchoro wenye Survey Plan D1.503/23 wa mwaka 1994.
Kiwanja hicho kina ofa iliyotolewa Aprili 18 mwaka 1964 kwa NHC ambao walikiuza kwa Moshi Majungu akiwa msimamizi wa mirathi ya baba yake Kondo Majenga.Abdi anadaiwa kununua kiwanja hicho mwaka 2004 kutoka kwa Moshi Kondo Majenga kwa niaba ya familia ya Kondo Majengo.Hata hivyo baada ya taratribu za mauziano hayo taratibu za kuhamisha miliki hazikukamilika.Imedaiwa kwa mara ya pili kiwanja hicho kiluzwa kwa tena na Moshi Mussa Majenga aliyeuwa msimamizi wa mirathi ya Kondo Majenga kwa Marshed mwaka 2008.
Baada ya mauziano hayo taratibu za kuhamisha miliki zilikamilishwa.
Katika hali ya kushangaza kiwanja hicho kilianza kutambulika kama kiwanja namba 1003 ambacho hakipo kabisa katika ramani ya eneo hilo lenye nyumba 490 tu.Inaelezwa Marshed alifanya upimaji pandikizi kwenye Survey D1.503/61 wa mwaka 2008 na kupata kiwanja kingine chenye namba 1003 juu ya kiwanja namba 212 hivyo kusababisha mgogoro mzito.
Kiwanja hicho wakati kinamilikiwa na NHC kilikuwa kinasomeka NHC/KIN/SEK/212.
Uchunguzi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa umebaini kuwepo mkataba batili baina ya Marshed na msimamizi wa mirathi kwa kutumia mkataba uleule aliotumia kumuuzia eneo Abdi mwaka 2004. Imebainika kiwanja namba 1003 kipo juu ya kiwanja namba 212 na kwamba usajili wa kiwanja namba 1003 chenye hati namba 105525 katika ofisi ya msajili hakina hati halali.
Kwa upande wa Halmshauri ya Manispaa ya Kinondoni, ilimuandikia barua Kamishna wa Ardhi ya Agosti 21, mwaka 2017, ikisainiwa na Rehema Mwinuka kwa niaba ya mkurugenzi yenye kumbukumbu namba KCM/LD/51043/65/ARR, kwenda Ofisi ya Kamishna wa Ardhi ili kiwanja hicho kufutwa.
Taarifa hiyo ya manispaa ilisema baada ya kupokea malalamiko ya Abdi, ikiwemo hukumu ya sheria namba 62/2009 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi, ofisi ilimtaka Abdi kuwasilisha malalamiko yake katika vyombo vya dola kama vile polisi na makama ili hatua stahili za kisheria zichukuliwe kwani jambo hilo linadalili za upatikanaji wa nyaraka na fedha kwa njia ya udanganyifu zisikokubalika.
Ilisema ofisi ya manispaa iliendelea kufanya uchunguzi na kubaini kiwanja namba 212 kiliuzwa mara mbili na kuita pande zote mbili kwa mazungumzo.“Baadhi ya wanafamilia waliofika katika ya manispaa walithibitisha kuuza nyumba yao iliyopo katika kiwanja namba 212 kwa Abdi na kukataa kutoa ridhaa ya kwa msimamizi wa mirathi kuuza nyumba hiyo na kwamba msimamizi huyo alighushi saini zao,”ilisema taarifa hiyo.
Pia ilieleza pamoja na kwamba Mahakama katika kesi namba 62/2009 ilimpa ushindi Marsged ofisi ya manispaa ilishauri hati iliyotolewa kwa Marshed ifutwe au iondolewe kwenye daftari la msajili wa hati na Abdi apewe haki yake.
No comments:
Post a Comment