Naibu Mkurungezi Mkuu wa Shirika la Ujasusi nchini Marekani FBI Andrew McCabe amefutwa kazi, siku chache kabla ya kustaafu.
McCabe amefutwa kazi na Mwanasheria Mkuu wa Marekani Jeff Sessions, ambaye amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya kiongozi huyo wa zamani wa FBI kufichua habari muhimu za siri.
Hata hivyo, McCabe amekanusha madai hayo na kusema amefutwa kazi kwa sababu alihusika katika uchunguzi wa iwapo Urusi iliingilia Uchaguzi wa urais mwaka 2016 na kumsaidia Donald Trump kushinda urais.
Rais Trump, amekuwa akimshtumu McCabe kwa kuegemea upande mmoja katika uchunguzi huo na kuwa upande wa chama pinzani cha Democratic.
No comments:
Post a Comment