A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 31, 2018

Mtu Mmoja anaedaiwa kuwa ni Jambazi auawa


JESHI la Polisi Kanda Maamlum ya Dares Salaam limemuua mtu mmoja anayedaiwa kuwa jambazi maeneo ya Buza jijini humo wakati akijaribu kuwatoroka askari alipokuwa akienda kuwaonyesha sehemu walipoficha sialaha na wenzake.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, RPC Lazaro Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa na bastola na alipohojiwa alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya ujambazi katika maeneo ya Mbagala na Kibiti.

“Tulipomhoji alikiri kuhusika na matukio ya ujambazi na kuwataja wenzake, aliahidi kutupeleka wanapoficha silaha maeneo ya Buza. Baada ya kukaribia eneo wanapoficha silaha hizo alianza kupiga makelele na kukimbia akijaribu kuwatoroka askari, polisi walimwamuru asimame lakini alikaidi.

“Polisi walifyatua risasi moja iliyiompata na kumjeruhi, baadaye alipoteza maisha na mwili wake kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi na kuhifadhiwa. Lakini wenzake tunawasaka kwa sababu aliwataja kwa majina na mahali wanapoishi.

Pia jeshi hilo linamshikilia Majid Abdallah (31) aliyekamatwa na bastola akiwa ameificha uvunguni mwa kitanda. Mambosasa amesema uchunguzi wa kesi hiyo unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages