A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 8, 2018

Matonya:Napenda Video zangu ziwe na tofauti na watu wengine wanavyofanya


Nyota mkongwe katika gemu ya Bongofleva, Matonya amedai hakujua kama amevalishwa vazi la kike 'Baibui' katika video yake mpya ya 'Kiherehere' ila alichokuwa anakihitaji yeye ni kuonekana tofauti na wasanii wengine.

Matonya amefafanua hilo kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya watu wengi kuanza kumfikilia ndivyo sivyo kutokana na kuonekana kuvaa vazi hilo angali yeye ni mtoto wa kiume.

"Napenda video zangu ziwe za tofauti na watu wengine wanavyofanya, navaa vitu fulani vya kipekee. Mimi niliambiwa kwamba hiki kitu ulichopiga siyo nikaona eenh sijui itakuaje, mashabiki zangu wasipate shida na mimi maana zile ni nashki kitu zimetengenezwa kwa ajili ya kazi ndio maana ma-sister zetu wanapiga jeans kali kabisa na inaweza ikawa ya 'boy friend' wake anaamua kuipiga kwaajili ya kunogesha na inamkaa vizuri", amesema Matonya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages