A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 30, 2018

Kajala afunguka ishu ya mahusiano yake na Chege

Msanii wa filamu nchini Kajala Masanja amefunguka na kuweka wazi kuhusu tetesi zinazosambaa kuwa sasa anatoka kimapenzi na msanii wa muziki wa Bongo fleva kutoka kiumeni Chege Chigunda.

Kajala akipiga stori na Big Chawa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio amekana kuhusu kutoka kimapenzi na msanii huyo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo na

"Mama yangu mzazi hakuna kitu kama hicho si mmeona Chege kapata mtoto juzi tu hapa, yaani mimi sina hata namba yake ya simu na haiwezi kutokea kitu kama hicho"alisisitiza Kajala

Mbali na hilo Kajala amewatakia kheri wanawake wote maarufu ambao wanakaribia kuolewa siku za karibuni na kusema kwake yeye badobado kwani anaamini mume mwema anatoka kwa Mungu hivyo atakapompata huenda na yeye ndiyo akafanya maamuzi hayo ya kuolewa sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages