Mauzo kwa wiki iliyoishia 16 March 2018 yalikuwa takribani shilingi bilioni
5 ikilinganishwa na mauzo ya shilingi milioni 518 kwa wiki iliyoishia tarehe 9 Machi 2018.
Vile vile Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliyoishia
tarehe 16
March 2018 ni hisa takribani milioni 3 ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya
laki 7 kwa wiki iliyoishia tarehe 9 Machi 2018.
Kampuni zilizoongoza
katika mauzo ya hisa kwa wiki iliyoishia tarehe 16 March 2018
ilikuwa kama ifuatavyo:
TCC……………………………………………86%
VODA …………………………………………….7%
CRDB………………………………………………4%
Mauzo ya Hati Fungani
(Bonds)
Mauzo ya hati
fungani katika wiki iliyoishia tarehe 16 Machi 2018 yalikuwa Shilingi bilioni
80.7 kutoka Shilingi Bilioni 65 wiki iliyopita ya 9 Machi 2018.
Mauzo haya
yalitokana na hatifungani kumi na moja (11) za serikali zenye jumla ya thamani
ya Shilingi bilioni 86 kwa jumla ya gharama ya Shilingi bilioni 80.7
Ukubwa Mtaji (Market
Capitalization)
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni zote zilizo orodheshwa katika soko umepanda
kwa Shilingi Bilioni 483 kutoka Shilingi Trilioni 22.7 wiki iliyopita hadi
Shilingi Trilioni 23.2 wiki iliyoishia tarehe 16
Machi 2018. Ongezeko hilo limetokana na kupanda kwa bei
za hisa za KCB (19%), USL (11%)TCC (7%) na pia
kuorodheshwa kwa hisa za kampuni ya TCCIA Investments Plc (TICL).
Ukubwa wa mtaji wa
kampuni za ndani zilizo orodheshwa katika soko la hisa umepanda kwa shilingi
bilioni 77 kutoka trillioni 10.2 hadi trilioni 10.3 ya wiki iliyoishia tarehe
16 Machi 2018. Ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa bei za hisa za TCC
(7%) na pia kuorodheshwa kwa hisa za kampuni ya TCCIA Investments Plc (TICL);
ambayo ukubwa wa mtaji wake ni shilingi bilioni 32.
Kampuni
|
16 Marchi 2018 (Shilingi)
|
9 Marchi 2018 (Shilingi)
|
Badiliko (%)
|
CRDB
|
170
|
190
|
-10.53%
|
DCB
|
380
|
380
|
0.00%
|
DSE PLC
|
1,400
|
1,580
|
-11.39%
|
MBP
|
600
|
600
|
0.00%
|
MCB
|
500
|
500
|
0.00%
|
MKCB
|
830
|
830
|
0.00%
|
MUCOBA
|
400
|
400
|
0.00%
|
NMB
|
2,750
|
2,750
|
0.00%
|
PAL
|
470
|
470
|
0.00%
|
SWALA
|
500
|
500
|
0.00%
|
SWIS
|
3,540
|
3,540
|
0.00%
|
TBL
|
14,000
|
14,000
|
0.00%
|
TCC
|
16,300
|
15,200
|
7.24%
|
TICL
|
0
|
0
|
|
TCCL
|
1,200
|
1,200
|
0.00%
|
TOL
|
780
|
780
|
0.00%
|
TPCC
|
1,480
|
1,480
|
0.00%
|
TTP
|
130
|
600
|
-78.33%
|
VODA
|
850
|
850
|
0.00%
|
YETU
|
600
|
600
|
0.00%
|
Kampuni
zilirodhodheshwa kutokea Masoko mengine
|
|||
ACA
|
4,790
|
5,370
|
-10.80%
|
EABL
|
5,380
|
5,360
|
0.37%
|
JHL
|
11,520
|
11,260
|
2.31%
|
KA
|
360
|
350
|
2.86%
|
KCB
|
1,140
|
960
|
18.75%
|
NMG
|
2,240
|
2,170
|
3.23%
|
USL
|
100
|
90
|
11.11%
|
Mtaji Jumla Makampuni
yote (Bilioni)
|
23,230
|
22,747
|
2.12%
|
Mtaji Jumla Makampuni
ya Ndani (Bilioni)
|
10,286
|
10,208
|
0.76%
|
Kiashiria cha DSEI
(pointi)
|
2,412
|
2,362
|
2.12%
|
Kiashiria cha TSI
(pointi)
|
3,923
|
3,894
|
0.74%
|
Ukubwa wa Mtaji wa Hatifungani
Hatifungani za
Serikali zilizoorodheshwa sokoni hadi kufikia tarehe 16 Machi 2018 zina ukubwa
wa jumla ya mtaji wa shilingi trilioni 8.35 na Hati fungani za makampuni
binafsi ni shilingi bilioni 98.
Viashiria (Indices)
Kiashiria cha kampuni zote
zilizoorodheshwa katika soko yaani DSEI kimepanda kwa pointi 50 kutoka pointi 2,362
hadi 2,412 pointi hii ikiwa ni kutokana na kushuka kwa bei za hisa za Kenya
Commercial Bank (KCB), Uchumi Supermarket ltd (USL) na Tanzania Cigarette
Company (TCC). Pia kishiria cha kampuni za ndani yaani TSI kimepanda kwa pointi
30 kutoka pointi 3893 hadi pointi 3923.
No comments:
Post a Comment