MIONGONI mwa wanamuziki wenye mchango mkubwa katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva ni Abdul Sykes ‘Prince Dully Sykes’ na huwezi kukosea ukisema Dully ni Bongo Fleva na Bongo Fleva ni Dully kwani hata kiumri amekuwa na muziki huo.
Alianza kufanya muziki akiwa chini ya miaka 15 na sasa ni zaidi ya miaka 15 akiwa kwenye gemu hilo na ngoma zake za sasa ukizisikiliza ni kama ameanza muziki huo jana.
Wakongwe wengi alioanza nao muziki na wengine waliomkuta wamekwishasahaulika kwenye gemu la Bongo Fleva. Lakini yeye bado anatesa na wimbo wake wa Bombardier wa hivi karibuni unadhihirisha uwezo wake.
Hata hivyo pamoja na uwezo wake mkubwa, mchango alionao kwenye muziki, mkali huyu hajaweza kutusua kihivyo kama walivyo baadhi ya wanamuziki ambao wameibuka hivi karibuni.
Kwa nini hajatusua? Hilo na majibu ya maswali mengine mengi mkali huyu anayajibu kwenye makala hii aliyofanya na Risasi Vibes.
Risasi Vibes: Dully kazi zinaendaje?
Dully: Safi tunapambana na changamoto za kila siku za muziki.
Risasi Vibes: Unaposema changamoto unamaanisha nini?
Dully: Kila siku muziki unabadilika, kwa hiyo ni lazima hata watu tubadilike pia maana usipobadilika muziki utakubadili.
Risasi Vibes: Wewe ni miongoni mwa wanamuziki wakongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, unaweza kutuambia nini siri ya kuzidi kudumu kwenye gemu?
Dully: Ni kipaji na rehemu za Mungu. Unajua mimi ni mwanamuziki na muziki ni maisha yangu. Sasa kila siku ninajitahidi kufanya muziki mzuri unaoendana na muda ili niweze kuzidi kudumu kwenye gemu.
Risasi Vibes: Unafikiri ni kwa nini wakongwe wenzako wamepotea kwenye gemu?
Dully: Kama nilivyosema awali, muziki unabadilika siku hadi siku. Kwa hiyo ni muhimu pale muziki unapobadilika na wanamuziki wabadilike kutokana na nyakati, kwani mabadiliko katika kila kitu kutokea ni lazima sasa mtu asipohitaji kubadilika basi ndiyo kama hivyo anaachwa nyuma. Hicho ndicho ninachoona kinawaponza wengi.
Risasi Vibes: Tukizungumza kipato chako kutokana na muda ambao umedumu kwenye gemu na idadi ya mashabiki wako unakusanya kama mkwanja kiasi gani?
Dully: Huwezi amini ninalipwa kiasi kidogo sana. Shilingi milioni moja, mbili, tatu mpaka nne. Kiukweli sijawahi kuchukua sijui milioni nane au kumi kwenye shoo. Nitakuwa nadanganya, kiasi kama hicho nimekuwa nikisikia wanachukua vijana walioibuka siku hizi. Kwa upande wangu mimi ni miongoni mwa wanamuziki wenye kipato cha chini kiukweli.
Risasi Vibes: Lakini pesa unayochukua pia sio ndogo, bila shaka unafanya shoo mara kwa mara na pia unamiliki Studio ya 4.12, pia bila shaka inakuingizia mkwanja?
Dully: Ni kweli pengine inaweza kuonekana siyo kiasi kidogo cha pesa na pengine siioni pesa kutokana na majukumu niliyonayo. Lakini hata hizo shoo unapata ngapi! Siyo kila siku utafanya shoo, na hata kwa studio pesa inayoingia siyo kihivyo. Ni kwa ajili ya kuweka tu mkate mezani.
Risasi Vibes: Unafikiri nini sasa sababu ya wanamuziki wa juzi kuingiza mkwanja mrefu kwenye shoo kuliko wewe?
Dully: Siwezi kufahamu kwa kweli. Lakini huwa kuna kitu kinanish-angaza sana, toka naanza muziki nime-kuwa mwana-muziki ‘peace’, sina shida na mtu, lakini kuna mastaa wa muziki huuhuu wananiwekea bifu. Sasa bifu sijui zinatoka wapi wakati hata pesa wanaingiza zaidi yangu!
Risasi Vibes: Ni mastaa gani hao wanaokuwekea bifu?
Dully: Aaah! Aachana nao lakini wapo nime-kuwa nikiw-asikia. Mwisho wa siku mimi ninadili na maisha yangu na si maisha ya mtu mwingine.
Risasi Vibes: Sawa, tumeona wakongwe wakiachana na ukapera na kuoa au kutambulisha wachumba wao, vipi kwa upande wako?
Dully: Nipo njiani. Nikiwa nataka kuoa nitamtambulisha huyo mke wangu. Lakini kwa sasa siwezi kufanya hivyo. Unajua wanawake wenyewe, unaweza kumtambulisha leo, mkaachana kesho, sasa utatambulisha wangapi. Lakini wakati unakuja pia nitatambulisha maana suala la kuoa ni la kheri.
Risasi Vibes: Kuhusu kazi sasa, vipi kuna lolote kwa mashabiki wako?
Dully: Kuna projekti ninamalizia na zikiwa tayari nitawafa-hamisha waweze kunipa sapoti.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Wednesday, March 21, 2018
Dully Sykes afunguka kuna mastaa wanamuwekea bifu
Tags
BURUDANI#
Share This
About kilole mzee
BURUDANI
Labels:
BURUDANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment