Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amepokea Tani 120 za Saruji ambazo ni sawa na Mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa Vyama vya ushirika 27 vya Mkoa huo vilivyoguswa na kempeni ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu Dar es salaam.
Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua Tofali 70,000 ambazo zitejenga ofisi 14 za kisasa kwaajili ya Walimu. Akipokea mifuko hiyo Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri ambapo amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na mwisho wa siku tuwe na wataalamu wa kutosha.
Aidha Bwana Tumaini amesema Ushirika utaendelea kuunga mkono kwa kila hali juhudi zinazifanywa na Rc Makonda

No comments:
Post a Comment