Rajabu Mohamed(kushoto) anayejifanya ni FREEMASON ambapo anafanya ukatili na unyanyasaji kwa wananwake ikiwa ni kuwapora pochi zao pamoja na kuwaibia fedha katika akaunti.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia, Rajabu Mohamed(25) anayejifanya ni Freemason ambaye amekuwa akifanya ukatili,unyanyasaji wa kijinsia na kupora mali hasa kwa wanawake na kuwatishia wanawake anaowafanyia ukatili huo kuwa wakitoa taarifa zake atawaua kwa kuwanyonya damu na kuwakata sehemu zao za siri.
Akizungumza leo kukamatwa kwa mtu huyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Februari 25 mwaka huu Polisi walimkata mtu huyo akiwa maeneo ya Mwenge ambako ndiko anakoishi na amekuwa akifanya vitendo hivyo vya kiakatili na vya kinyama kwa kujifanya Freemason.
Amesema mtu huyo amekuwa akitumia gari naomba T 172 BLH aina ya Fun Cargo rangi ya Silva ambapo amekuwa akikamata wanawake kwa kuwalaghai kuwa ni mfanyabiashara na wakishaingia kwenye gari lake hutumia nguvu na kuwanyang'anya vitu vilivyomo kwenye mabegi hayo na kuanza kuwazungusha barabarani huku akiwatisha kuwa yeye ni Freemason na kuwa atawaua kwa kuwanyonya damu au kukata sehemu zao za siri.
"Kupitia vitisho hivyo huwalazimu wotoe namba za siri za simu zao na kuchukua kadi zao za benki na kuwaibia fedha zao kwenye ATM na baada ya hapo kuwashusha na kuwatelekeza kwenye vichochoro huyu mtu tumemuhoji anasema kwa sasa ameacha,ukimuangalia sura yake ni ya binadamu lakini ni mnyama wa hali ya juu kabisa.Amefanya mambo mengi ya kishenzi, tunaendelea na taratibu nyingine na baada ya hapo atapelekwa mahakamani ili ajibu tuhuma za makosa ambayo yanamkabili ,Sheria tunataka ichukue mkondo wake,"amesema Kamanda Mambosasa.
Ameongeza kuwa matukio ambayo anatuhumiwa kufanya mtu huyo kwa baadhi yawanawake ambao wametoa taarifa zake hata mnyama ambaye yupo mbugni na wanyama wezake hawezi kufanya kwani ni vitendo vya kinyama na kikatili ambavyo binadamu hawezi kuvifanya.
Amesema kuwa iwapo atakuwa na Ukwimwi maana yake atakuwa ameambukiza wanawake wengi na hafai kabisa kwenye jamii hivyo ni lazima sheria ichukue mkondo wake aweze kupata adhabu kutokana na makosa hayo.
Aidha Kamanda Mambosasa ametoa wito kwa watu ambao wamefanyiwa ukatili na mtuhumiwa huyo kufika polisi kutoa taarifa kwa mtu huyo si mwema hata kidogo ingawa sura yake ni ya kibinadamu.
"Nitoe rai kwa wale waliofanyiwa ukatili kufika kituoni kutoa taarifa wasiogope wanaweza kufika hata kwenye wmadawati yetu ya polisi ili kutoa taarifa"Amesema Mambosasa.
No comments:
Post a Comment