A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, February 27, 2018

Tanzania kuja na mpango wa kuepukana na saratani ya mfuko wa uzazi.

Wadau mbalimbali wa afya kwa kushirikiana na Wizara ya afya nchini leo wamekutana kwa pamoja kwa lengo la kupena taarifa kuhusu chanjo ya saratani ya mlango wa uzazi sambamba na kupanga mikakati na kupanga ni kwa kiasi gani wanaweza kufanikisha mpango wa utaoji wa chanjo hiyo ndani ya nchi nzima.

Akiongea waziri mwenye dhamana ummy Mwalimu amesema kuwa wanategemea kuzindua rasmi utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ifikapo April mwaka huu ambapo wasichana walioko Kati ya umri wa miaka 14-18 watapa chanjo na kuongeza kuwa zitatolewa dozi mbili ambapo dozi ya pili itatolewa baada ya miezi sita Mara baada ya kupata dozi ya kwanza.

Pia Ummy amesema kuwa chanjo hiyo itagharimu sh.30000 za kitanzania na kuwatoa hofu watanzania kwa kusema kuwa serikali kwa kushirikiana na Wizara ya afya wanahangaika ili kuhakikisha kuwa inafika hatua chanjo hiyo inatolewa bure bila malipo.

Aidha amebainisha kwamba kwa mwaka huu wamedhamiria kutoa chanjo kwa wasichana 616,734 na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wanawalinda wasichana wote wenye umri kuanzia 9-14 dhidi ya ugonjwa wa saratani ya mfuko wa uzazi na kuongeza kuwa watajitahidi kuwa na takwimu sahihi za watoto wa kike wanaozaliwa ili kuweza kufikia lengo.

Pia ametaja maeneo ambayo chanjo hiyo itakuwa inapatikana kuwa ni katika vituo vya afya, katika baadhi ya shule zitakazochagukiwa na kwa baadhi ya maeneo ndani ya jamii.

"Chanjo hii itatolewa kwenye vituo vya afya, kwenye baadhi ya shule zitakazochaguliwa na baadhi ya maeneo yaliyopo ndani ya jamii' amesema Ummy.

Lakini amewatoa hofu wananchi juu ya chanjo hiyo na kusema kuwa imethibitishwa na WHO kwa kushirikiana na TFDA hapa nchini na haina madhara yoyote na inafaa kwa matumizi ya binadamu na kuahidi kwamba ataanzisha kampeni yeye kama mama ili kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi Mara tu zoezi la utoaji wa chanjo litakapoanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages