Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya
ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Baraza
Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA ambapo amefurahishwa na kasi ya ujenzi huo.
Ujenzi wa jengo hilo la kisasa ni jitiada za RC Makonda
kuthamini na !kuwapa heshima Viongozi wa Dini kwa kuhakikisha wanafanyakazi
katika mazingira mazuri na yenye hadhi kutokana na thamani na mchango wao
mkubwa katika jamii.
Jengo hilo la kisasa lenye Gorofa Nne pamoja na Ground floor
lina Ofisi ya Mufti wa Tanzania, Ofisi ya katibu, VIP room, kumbi za mikutano,
Ofisi za wafanyakazi, ofisi za mshauri,Jiko,Vyoo, sehemu ya Kufanya Dua pamoja
sehemu ya Mapokezi.
RC Makonda amesema kazi wanayofanya Viongozi wa Dini ni kubwa
hivyo tunapaswa kuthamini kwa kuwaweka mazingira mazuri ya kufanya kazi.
Aidha RC Makonda amesema shauku yake ni kuona hadi mwezi wa
Ramadhani jengo linakuwa limekamilika na kuanza kutumika.
Aidha RC Makonda amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea
Amani Taifa na viongozi wake.
Kwa upande wake Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber
amemshukuru RC Makonda kwa kuwajengea jengo hilo na kusema katika Miaka 50
BAKWATA haijawahi kuwa na jengo zuri na lakisasa Kama hilo hivyo RC Makonda
anaweka historia ya kwanza.
Mufti amesema jengo lililokuwepo lilikuwa likiwafanya kuona hata
haibu hata kupokea ugeni wa viongozi wa kislamu ulimwenguni.
Katika ziara hiyo Viongizi wa Dini kwa pamoja wamemuombea Dua RC
Makonda pamoja na Rais Dr. John Magufuli kwa kuwezesha kujengwa kwa msikiti wa
Mfalme wa Morocco wenye uwezo wa kuchukuwa watu 8,000 ampapo ujenzi
unaendelea.
MATUKIO KATIKA PICHA RC MAKONDA AKIKAGUA UJENZI HUO
Makonda akiwasili katika ofisi zinazojengwa
Rc Makonda akisalimiana na Shekh Mkuu wa Tanzania
Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Rc Makonda akipata maelezo kutoka kwa mafundi wa ujenzi huo
Ukafika wakati wa dua kuombea ujenzi huo usiwe na vikwazo
No comments:
Post a Comment