Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na
wananchi walimu pamoja na wanafunzi katika shule ya msingi Mbande iliyopo
katika Halmashauri ya temeke nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam alipofanya
ziara ya kukagua mpango mkakati wa
halmashahuri hiyo wa kutatua changamoto zilizopo katika shule za Msingi Mbande
na maji matitu zenye wanafunzi wengi waliojitokeza kujiandikiasha na darasa la
kwanza kwa mwaka 2018. (kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na kulia ni Diwani wa kata hiyo Hemmed Karata,
pamoja na viongozi wengine wa kata hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva (kulia) akizungumza na
wanainchi walimu pamoja na wanafunzi katika shule ya msingi Mbande iliyopo
katika Halmashauri ya temeke nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye ziara
ya Mkuu wa Mkoa alipofanya ziara ya
kukagua mpango mkakati wa halmashahuri hiyo wa kutatua changamoto zilizopo
katika shule za Msingi Mbande na maji matitu zenye wanafunzi wengi
waliojitokeza kujiandikiasha na darasa la kwanza kwa mwaka 2018.wa tatu kushoto ni Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kulia kwa Makonda ni Diwani wa kata ya Kirungule Saidi Fella na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo.
Kaimu Afisa Elimu Msingi Sylvia Mutasingwa, akitoa taarifa
ya uandikishwaji wawanafunzi wa darasa
la kwanza mwaka 2018kwakuwa imeonesha
kuwa wilaya hiyo inaongoza kwakuwa na wanafuzi wengi katika shule ya msingi Mbande
iliyopo katika Halmashauri ya temeke nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwenye
ziara ya Mkuu wa Mkoa alipofanya ziara
ya kukagua mpango mkakati wa halmashahuri hiyo wa kutatua changamoto
zilizopo katika shule za Msingi Mbande na maji matitu zenye wanafunzi wengi
waliojitokeza kujiandikiasha na darasa la kwanza kwa mwaka 2018
Mkuu wa Mkoa akiwasili katika shule ya msingi Mbande
akiongozana na baadhi ya viongozi mbalimbali alioambatana nao katika hafla hiyo
Baadhi ya wakazi wa Mbande pamoja na wanachama wa Chama Chamapinduzi walijitokeza katika hafla hiyo
Wanafunzi wa darasa la kwanza wakiwa katika hafla hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwaaga wanafunzi wa shule ya
msingi Maji Matitu iliyopo mbagala
Wananchi wa Mbande wakisindikiza gari ya Mkuu wa Mkoa kwa furaha baada yakumaliza
ziara yake shuleni hapo.
Mkuu Wa Wilaya ya Temeke Félix Lyaniva (kulia) akizungumza na wanafunzi pamoja na walimu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wakuu wote wa Idara mbalimbali hususani katika sekta ya Elimu kutekeleza majukumu yao ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Rc Makonda ameyasema hayo leo alipofanya Ziara katika shule ya msingi Majimatitu na Shule ya Msingi Mbande zilizopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salam na kuangalia mpango mkakati wa halmashauri hiyo katika kutatua changamoto zilizopo katika shule hizo ambapo wanafunzi walioandikishwa kwa mwaka 2018 idadi imekuwa kubwa na kupelekea uhaba wa miundombinu katika shule hizo.
Amesema ni wakati kwa wakuu wa idara katika sekta ya Elimu kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya Elimu ili kusaidia elimu inakuwa kwa kiwango kikubwa na kutengeneza kizazi cha wasomi kwani elimu ni chachu ya maendeleo katika Jamii.
"Wakuu wa idara yapasa kuamka na kuweza kufuatilia kwa Mkurugenzi wako na kuweza kuatatua changamoto zote zilizopo katika idara yako nisisikie Mkuu wa Idara anasema nimeshindwa kutekeleza huu ni wito Wangu kwenu wakuu wote wa Idara zote katika Mkoa wangu"Amesema Rc Makonda.
Aidha Makonda ametoa wiki mbili kwa Mkurugenzi wa manispaa hiyo pamoja na Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanatafta eneo la kuweza kujenga shule nyingine ambapo amesema baada ya kupatikana eneo hilo Ujenzi wa shule nyingine ya Mbande itakayosaidia kutatua changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo.
"Natoa wiki mbili kwa Mkurugenzi pamoja na Mkuu wa Wilaya kuhakikisha eneo linapatikana la kujenga shule nyingine ya Mbande na mimi mwenyewe nitakuja kujenga msingi kabla ya tarehe 10 mwezi ujao niwe nimepata taarifa ya eneo hilo kupatikana ili tujenge shule nyingine"Amesema Makonda.
Katika shule ya Msingi Majimatiti wanafunzi walioandikishwa darasa la kwanza ni 976 ambapo idadi ni kubwa na katika shule ya Mbande pia idadi ya wanfunzi walioandikishwa kwa mwaka huu ni kubwa kuliko shule zote za Mkoa huo, ambapo wanafunzi walioandikishwa ni 1,132 n'a bado uandikishaji unaendelea hadi March 30 mwaka huu.
Amesema halmashauri zinapaswa kuaandaa mpango mkakati wa muda mrefu wa za kuratatua changamoto hizo kwa kujenga shule pamoja na vyumba vya madarasa ili kusaidia n'a kuhakikisha changamoto kama hizi hazijitokezi tena na kuweza kuboresha sekta ya Elimu na kutengeneza kizazi kilicho bora chenye kuleta maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.
Akitoa taarifa ya jumla ya Wilaya kielimu kwa mkuu wa Mkoa kaimu Afisa Elimu msingi wilaya ya Temeke Slyvia Mutasingwa amesema manispaa hiyo inajumla ya wanafunzi 1,6625 , wavulana 81,718 wasichana 84,387 na Walimu 3,018 Wanaume 554 Wanawake 26,032 na kusema kuwa Manispaa hiyo inaupungufu wa vyumba vya Madarasa 1,565 huku mahitaji halisi yakiwa ni 3,718 na kufanya kuwa na upungufu vyumba 2149 na upungufu wa matundu vya vyoo 2,219 kwa Mbande pekee kuna mahitaji ya madarasa 153 madarasa yaliyopo ni 38 kunaupugufu wa madarasa 115, kwa upande wa matundu ya choo kuna matundu 40 huku mahitaji halisi yakiwa ni 310, na kuna madawati 2298 yalipo ni 1990 kuna upungufu wa madawati 308.
No comments:
Post a Comment