A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, February 7, 2018

Mashabiki wa Simba waombwa kujitokeza kwa wingi kuipa timu nguvu


Uongozi wa klabu ya Simba umewaita mashabiki wake kwenda kwa wingi kwenye uwanjani kuwaunga mkono ili waimalize Azam FC.

Simba ina kibarua cha kuivaa Azam FC katika mechi yake ya pili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mara amesema wanawategemea mashabiki kama sehemu ya mafanikio na vema wajitokeze kwa wingi kuhakikisha wanawaunga mkono.

"Timu iko tayari baada ya mazoezi mepesi leo, tunawaomba wanachama na mashabiki waje kwa wingi wakiwa na jezi zao.

"Wao ni muhimu sana kwa kuwa ni sehemu ya hamasa ya ushindi. Azam ni timu nzuri, tunajua na tunaheshimu timu yao lakini tuna kikosi kizuri," alisema.

Manara amesema bado ligi ni mbichi na lazima wajitume zaidi kuhakikisha wanafanya vema zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages