Kocha wa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Goerge Lwandamina, amemwacha nje ya kikosi cha leo mchezaji wa timu hiyo Ibrahim Ajib kwenye mchezo wa leo dhidi ya Lipuli FC.
Ajib ambaye anashika nafasi ya pili kwa ufungaji msimu huu ndani ya klabu hiyo hajaripotiwa kuwa ameachwa kwa sababu gani huku ikiwa ni mechi ya pili sasa ambapo aliachwa kwenye mchezo wa Kombe la shirikisho dhidi ya Ihefu FC.
Kwa upande mwingine daktari wa timu hiyo Dr. Bavu amethibitisha kuwa mlinzi wa kati Abdallah Shaibu 'Ninja' atakuwa nje kwa wiki 3 au 4 baada ya kuumia kwenye mashindano ya kombe la Mapinduzi.
Dr. Bavu ameeleza kuwa awali walijua ni tatizo dogo lakini baada ya uchunguzi wa kina tumegundua kuwa kuna tatizo kwenye kisigino na kifundo cha mguu wa kushoto.
Yanga leo inakutana na Lipuli FC kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa kwenye mchezo wa raundi ya 16 ligi kuu soka Tanzania Bara. Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 28 wakati Lipuli FC ikiwa na alama 16 katika nafasi ya saba
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, February 3, 2018
Ibrahim Ajib atupwa nje ya uwanja
Tags
MICHEZO#
Share This
About kilole mzee
MICHEZO
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment