Meneja Masoko wa Kampuni ya GSM Farida Rubanza
(kulia), akizungumza na wandishi wa habari katika hafla ya
utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni hiyo na kampuni ya Danube
Home inayojishughulisha na biashara ya kuuza samani
ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda
kikubwa cha kutengeneza Samani za ndani katika eneo la
Kigamboni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wanne kushoto ni Waziri wa Viwanda , Biashara
na Uwekezaji, Charles Mwijage pamoja na
maofisa wengine kutoka GSM na Danube.
Waziri wa
, Biashara na Uwekezaji,
Charles Mwijage (wa pili kushoto), akizungumza katika hafla ya utiaji sahihi makubaliano kati ya
kampuni za GSM na Danube Home inayojishughulisha
na biashara ya kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo
watajenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza
Samani za ndani katika eneo la Kigamboni nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushotoni
Mkurugenzi Mtendaji wa Danube Home, Sayed Habib, wapili
kulia ni Rais wa Danube Home Tanzania, Ghalib Mohamed na Meneja
Masoko wa GSM, Farida Rubanza. Hafla hiyo ilifanyika kwenye duka la Danube,
Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Danube Home,
Sayed Habib (katikati), akizungumza
na wandishi wa habari katika ya utiaji sahihi makubaliano kati ya kampuni za
GSM na Danube Home inayojishughulisha na biashara ya
kuuza samani ambapo kuptia makubaliano hayo watajenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza
samani za ndani katika eneo la Kigamboni nje
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
wa GSM, Fahad Ahmad pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Charles Mwijage ambae
ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam
leo.
Waziri wa Viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage ambae ndio alikuwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo akisalimiana na mmoja ya wawekezaji kwenye Kampuni
ya Danube Home Raymond Healy, wengine ni Maofisa wa Kampuni hiyo.
Waziri wa Viwanda
amezipongeza kampuni za GSM na DANUBE Kuweza kuungana na kutaka kuanzisha
kiwanda kitakachotengeneza samani mbalimbali hapa nchini.
Waziri Mwaijage
amezungumza leo katika tukio la makubaliano na kati ya kampuni zote mbili
ambapo zimekubali kuungana na kuamua kutengeneza kiwanda kitakachozalisha
samani mbalimbali ili kuwapa wananchi fursa ya kupata bidhaa kwa ukaribu na kwa
bei nafuu .
Amesema serikali ipo
tayari kuwatoa sapoti katika kuhakikicha kiwanda hicho cha kuzalisha samani
kinakuwepo nchini ambapo amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kuyapeleka
watanzania kupata ajira na kusaidia kukuza uchumi wa viwanda.
"Nafahamu
kyanzishwa kwa kiwanda hichi kwanza mmenisaidia mimi katika kutekeleza sera ya
kukuza uchumi wa viwanda, pia itatengeneza ajira kwa wananchi wetu hivyo ni
jambo jema na napenda kiwanda hichi kianzishwe" amesema Mwaijage.
Aidha amebainisha kuwa
kutengenezwa kwa samani katika nchi yetu kitasaidia kukuza soko la biashara na
wateja kupata bidhaa kwa bei nafuu na kwa urahisi zaidi.
Kwa upande wake Meneja masoko wa Kampuni ya GSM , Farida Rubanza amesema wana tarajia kujenga kiwanda kikubwa kitakacho kuwa kina tengeneza samani za ndani (Furniture) kwa ajili ya kuuza nchini na kusafirisha nchi mbalimbali duniani.
‘’Sisi GSM na DANUBE tumeona Nivema tukaungana ilikujenga kiwanda hapahahapa na tutakuwa tuna pata malighafi hapahapa na kiwanda kikikamilika tuta kuwa na uwezo wa kuuza Contener 500 kwa mwezi na tutauza masoko ya nje na ndani ‘’ alisema .
Rubanza pia ame mshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe. John P.Magufuli na serikali yake kwa kwa kuweka mazingira Rafiki kwa wawekezaji wa ndani na wa kigeni na kuahidi kuwa wao kama waekezaji wataendelea kutoa ajira kwa watanzania.
Katika muungano huu amesema, wataanzisha DUNUBE home Academy na watachukua wahitimu wa vyuo nchi na watawafundisha na kuwapatia ajira ndani na nje ya nchi walikowekeza na wemgine watawa tafutia ajira sehemu mbalimbali
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa kampuni ya DANUBE Home Sayed Habib amesema wamewiwa kuja kuwekeza Tanzania kwani
ina rasilimali za kuweza kusaidia uzalishaji wa samani hizo.
Ameishukuru kampuni ya
gsm kukubali kufanya muunganiko utakaosaidia kuanzishwa kwa kiwanda icho hapa
nchini.
Baadhi ya waandishi wakiwa kazini katika hafla hiyo
Majadiliano yakiendelea
Waziri akitoka katika duka hilo
Maofisa wa Danube wakiwa katika picha
Baadhi ya bidhaa zinazopatikana katika duka la danube
No comments:
Post a Comment