Mzee Waziri akionesha hati halali ya umiliki wa nyumba hiyo
Hili ni eneo la nyumba la mzee huo.
Hili ni eneo la nyumba la mzee huo ambalo ndio alilozulumiwaHapa akiwa katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Ili kupata msaada wa kisheria
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya Saba hapa nchini adhulumiwa nyumba na mpangaji wake,baada ya kuuziwa na Mtu aliyetapeli nyumba hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya huyo mstaafu Waziri Juma amesema nyumba hiyo alikuwa akimpangisha mpangaji huyo ambaye Ni mchina,na alaikuwa akilipa kodi Kama ipasavyo lakini baada ya Muda akadai kuwa ameuziwa nyumba hiyo.
"Hii nyumba Ni kiinua mgongo changu na niliamua kuipangisha ili niweze kupata hela ya kunisaidia kimaisha katika wakati huu niliostaafu lakini nimedhulumiwa na mchina akidai ameinunua "amesema Juma Waziri.
Aidha amebainisha kuwa kabla ya mpangaji huyo kuinunua nyumba hiyo ilikopwa fedha benki na Mtu asiyefahamika na walipofahamu walitoa taarifa kwa benki hiyo wasitoe mkopo huo lakini baadae ikaja onekana ilikopwa hela kwa nyumba hiyo kitu ambacho kiliwashangaza Sana
Anaendelea kusema kuwa baada ya fedha hiyo kukopwa na Mtu asiyefahamika na ambaye Hakuna mwanafamilia alishindwa kurejesha mkopo huo,na kupelekea nyumba hiyo kuuzwa ili kulipa deni hilo la benki ndipo mpangaji huyo ambaye ni mchina aliinunua.
"Mimi binafsi sijawahi kukopa benki wala kuuza nyumba maana hii nyumba inanisaidia kujikimu kipindi hiki cha uzeeni hivyo Naomba hawa walipfanya kitendo hiki waweze kuchukuliwa hatua."Amesema Juma.
Kwa upande wa watoto wa Mzee huyo wamelaani kitendo hicho na kuomba wahusika kuchukuliwa hatua Kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment