A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, January 30, 2018

Yanga SC kushuka dimbani Leo kukipiga na Ihefu FC



Mabingwa wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, klabu ya Yanga SC leo inashuka dimbani kuvaana na timu ya Ihefu FC ya Wilayani Mbarali  jijini Mbeya kwenye mchezo wa hatua ya 32 ya michuano hiyo.

Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara utaifanya Yanga itolee macho zaidi mechi ya leo ili iweze kusonga mbele kwaajili ya kuusaka ubingwa ili kujihakikishia uhakika wa michuano ya kimataifa mwakani. Hadi sasa Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Simba na Azam FC.

Michuano hiyo ambayo bingwa wake huwa anapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa leo itashuhudiwa mechi saba zikichezwa katika viwanja tofauti.

Klabu ya Ihefu imetinga hatua hii ya 32 baada ya kuitoa Mbeya City katika hatua iliyopita hivyo mechi haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa kikosi hicho ambacho kitakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya.

Tayari bingwa mtetezi wa michuano hiyo Simba SC ameshaondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kichapo kutoka kwa timu ya Green Worriors ya Dar es salaam kwenye hatua iliyopita.

Ratiba kamili ya leo

Ihefu FC Vs Yanga SC
JKT Tanzania Vs Polisi Dar
Polisi Tanzania Vs Friends Rangers
Shupavu FC Vs Azam FC
Ndanda FC Vs Biashara
Kariakoo Lindi Vs Mbao FC
Kagera Sugar Vs Buseresere

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages