Kampuni ya UmojaSwitch leo imechezaesha droo yake ya
bahati nasibu ya Shinda na Umoja kwa
wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8
Januari mwaka huu ambapo zaidi ya
wateja 25 wameibuka washindi katika droo ya leo.
UmojaSwitch ilianzisha bahati nasibu hiyo ya Shinda na Umoja mwezi Desemba mwaka jana kwa lengo la kutoa
hamasa kwa wateja wao kupitia kampeni yao ya kubadili kadi za UmojaSwitch kutoka
kwenye mfumo wa zamani na kwenda kwenye mfumo mpya wa ‘Microchip’
Katika makundi matatu yaliyo chezeshwa leo kundi la kwanza limetoa washindi 25 waliojishindia T-Shirt za UmojaSwitch,
Mzunguruko wa pili umetoa washindi wa tano wa Simu
za Mkononi (Smart Phone), mzunguruko wa
tatu umepata washindi wawili wa fedha taslimu mara mbili ya fedha walizokuwa
wanatoa kwenye Akaunt zao kupitia kadi za UmojaSwitch na Mzunguzuro wa nne umepata
mshindi mmoja aliejishindia kiasi cha Shilingi Milioni Moja Taslimu.
Akiendesha Droo hiyo Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Bi
Beatrice Emmanuel Chini ya
Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari Maggid amewapongeza
washindi wa zawadi hizo na kudai kuwa watafanya
mawasiliano na Benki husika wanazotumia washindi wao ili kuweza kuwapatia
zawadi zao muda mchache kuanzia leo.
Aidha Beaterice amewataka wateja ambao bado
hawajabadilisha kadi zao za awali kufika
kwenye Benki husika ili kubadili kadi zao na kuwea kuingia katika bahati nasibu
hiyo ya Shinda na UmojaSwitch kwenye droo inayofuata.
Kampuni ya UmojaSwitch inaunganisha mabenki zaidi ya
27 Tanzania kwa lengo la kushirikiana kutoa fedha kwa njia ya kilectronic ya
ATMs
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel (kushoto)
akibonyeza kitufe kuashiria kuchezesha droo ya bahati nasibu ya Shinda na Umoja
kwa wateja wake zaidi ya 32,222 waliotumia
kadi za UmojaSwitch kati ya tarehe 1- 8 Januari mwaka huu ambapo zaidi ya wateja 25 wameibuka washindi
katika droo hiyo hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika katika ofizi zao
jijini Dar es Salaam leo (kulia) ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo yakubahatisha Bakari
Maggid
Afisa Masoko wa UmojaSwitch Beatrice Emmanuel akizungumzana waandishi wa habari katika hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment