Wanawake wametakiwa kujiamini, kuthubutu, kujishusha, kuwa wanyenyekevu na wabunifu katika biashara zao ili kufikia malengo mbalimbali waliyojiwekea na kwa Taifa kiujumla.
Hayo yamesemwa Na mkurugenzi wa IPP media Regional Mengi alipokuwa akizungumza na chama cha wanawake wafanyabiashara Na wajasiliamali(TWCC) waliokutana katika semina ili kujadili masuala mbalimbali kuhusiana na chama chao pia kuboresha bidhaa zao ili kufikia malengo waliyojiwekea ambapo amewataka wanawake kuwa Na macho ya kuona fursa ili kuzidi kujiingizia kipato ,kujiamini,kuendana Na Na teknologia.
Aidha Mengi amewaonya wanawake kuwa kuwataka waache majivuno badala yake wawe wanyenyekevu ili kuongeza wigo wa kukuza biashara na amehitimisha kwa kuwakabidhi jengo kwaajili ya kufanyia shughuli zao pamoja na kujifunzia shughuli mbalimbali.
Naye mkurugenzi wa uwezeshaji Baraza la Taifa la wananchi kiuchumi bi.Anna Dominic amesema Baraza litaanza kutoa mikopo kupitia saccoss walioianzisha
Naye mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara Na wajasiliamali(TWCC)bi.Jacline Mnenea amemshukuru Mengi kwa kuwakabidhi jengo hilo kwaajili ya kufanyia shughuli zao pamoja Na mafunzo mbalimbali kwani kutawasaidia kufanyia Nazi zao kwa weledi.
No comments:
Post a Comment