WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo
cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kufuatia
hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike
ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo
hicho.“Serikali
haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA
aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga
kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua
kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Mara.Waziri
Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango.
Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.
Waziri
Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi
kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa
zimebanduka.Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya
shughuli zao za kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara
za magendo.
Waziri
Mkuu amesema magendo yanaikosesha Serikali mapato, hivyo bidhaa yoyote
itakayokamatwa ikiingizwa nchini kwa njia za magendo itataifishwa pamoja
na chombo cha usafiri kilichotumika. Pia
Waziri Mkuu ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega,
ambapo amewasisiza wananchi wasimamie elimu ya watoto wa kike ili
wafikie malengo yao.
Amesema
Serikali imeweka sheria kali kwa yeyote atakayekatisha masomo kwa watoto
wa kike iwe kwa kumpa ujauzito au kumoa, adhabu yake ni kifungo cha
miaka 30 jela. Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze
kutimiza ndoto zao na kamwe wasijihusishe katika mambo ambayo
hayahusiani na masomo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 17, 2017.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimu wagonjwa wakati alipotembela
hospitali ya wilaya ya Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Mara,
Januari 17, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adm Malima.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimfariji mtoto Naomi Ogaja (3)
aliyelazwa katika hospitali ya walaya ya arime kwa matibabu wakati
alipotembelea hospitali hiyo Januari 17, 2017. Kshoto ni baba mzazi wa
mtoto huyo Ogaja Wajangwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la
Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake
na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika
Januari 17, 2018. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adama Malima.
(Picha na Ofisi Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi baada ya kukagua jengo la
Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Sirari na kueleza kutorihishwa kwake
na viwango vya ujenzi wa jengo hilo (pichani) ambalo limeanza kuharibika
Januari 17, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la Kituo cha Afya
cha Sirari wilayani Tarime Januari 17, 2017. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Boreha wilayani Tarime, Januari 17, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maeneo na majengo ya Shule ya Sekondari
ya Wasichana ya Borega wilayani Tarime baada ya kuifungua akiwa katika
ziara ya mkoa wa Mara Januari 17, 2018.
No comments:
Post a Comment