Dar Es Salaam.
Baada ya Sakata la Mjane Bi.Benadetha Rwendela kufanyiwa Dhulma ya nyumba yake iliyopo Mtaa wa Kondo, Kata ya Kunduchi,kwa kupiga Mnada, ambapo leo familia nyingine ya aliyekuwa Kigogo Mkubwa Kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu, Bw.Edward Bejumla, imeibuka na keleza juu ya utaperi wa nyumba yao waliofanyiwa.
Bi.Stella Bejumla Akiongea kwa Majonzi mbele ya waandishi wa Habari,baada ya kudai kudhulumiwa Nyumba yao.
Leo Hii KILOLE MZEE BLOG imeshuhudia Familia hiyo ikimlilia Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuwaomba iwasaidie kupata haki yao ambayo wamedai wamedhulumiwa na Bwana Aloycious Gonzage Mandago.
Banjumla ambaye ni Mfanyakazi mstaafu wa cheo cha uhakikimali Mkuu wa Serikali na mkewe Stella, ambaye ni Ofisa Mstaafu wa Maktaba Kuu ya Taifa, wamedai kutaperiwa nyumba iliyopo Kitalu namba 91 Block B, eneo la Tegeta, Mtaa wa Bahari Beach, jijini Dares Salaam.
Mandago Ambae kwa sasa Mtuhumiwa wa pili katika kesi ya utakatishaji fedha ambao umeisababishia Serikali ya Tanzania hasara ya Shilingi Bilioni 15.
Bw.Edward Bejumla akizungumza na Waandishi wa Habari Dhidi ya sakata hilo.
Kwa mujibu wa Bajumla, alisema, sakata la kutaperiwa nyumba hiyo, imesababisha mama yake kufariki ghafra kwa mshituko mwaka 2014.
Alisema baada ya kutaperiwa na kufukuzwa katika nyumba kisha vyombo vyake kuharibika, kwa kutupwa nje na vingine vikiachwa huku vikinyeshewa na mvua ambapo pia amedai alikuwa akimficha mama yake mzazi lakini watu walimpenyezea taarifa hiyo na aliposikia alipata mshituko na kufa papo hapo.
Hii ndiyo nyumba ambayo wanaishi kwasasa,huku wakidai kuwa kwasasa wameishiwa hata kodi ya kulipia pango hilo.
“Mama alikufa kwa mshituko baada ya kupewa taarifa kuwa maisha yangu yamesambaratika na nimekuwa masikini.Nahisi hakuamini ila alifariki papo hapo,” alisema Bajumla.
Huu ni Mkataba wa mauziano (Sale agreement) ambao wanadai kuwa ni feki.
Amesema, Pesa hizo alichukua mkopo katika benki ya CRDB ambapo alishindwa kumalizia deni la sh. milioni 20 la mkopo huo na kupelekea kuanza kutafuta msaada.
Huu ni mwonekano kwa Nje wa Nyumba yao ambayo wamedai kuwa wamedhulumiwa.
“Wakati nahangaika kutafuta fedha za kumalizia mkopo kuna rafiki yangu wa karibu alinishauri nimuone Mandago kwani huwa anatoa msaada kwa makubariano ya kumuongeza riba,” alisema Bajumla.
Ameeleza kuwa ,alifika kwa bwana Mandago, ambaye alikubari kulipa deni hilo kwa mkataba maalumu na kuwataka kuwasilisha nyaraka muhimu za nyumba yao ambapo walifanya hivyo.
Bajumla amesema kuwa baadae aliwasilisha nyaraka za nyumba, Mandago alianza kuwakimbia kwani kila walipokuwa wakimfuata ofisini kwake walibiwa kuwa yuko nje ya nchi.
“Juni mosi mwaka 2015 tuliamua kwenda Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Tulimuona Waziri Williamu Lukuvi ambaye baada ya kutazama alibaini nyumba hiyo imabadilishwa ummiliki na kwamba ilikuwa imeuzwa,” alisema Bajumla ambaye amepata matatizo ya kiafya kutokana na sakata hilo.
Aidha amesema , walishangazwa kusikia nyumba yao ilikuwa imebadilishwa hati na kumwinda Mandago na kufanikiwa kumpata.
“Tulimwambia atupe nakala za mkataba wa mauziano alikataa na kueleza kuwa tulisaini mkataba wa mauziano kwa sh.milioni 96.Kwamba tulimuuzia nyumba hiyo kwa fedha hizo jambo ambalo si kweli,”alieleza Bajumla.
Alisema nyaraka Nyaraka hizo zinazoonyesha mkataba wa mauziano na Mandago walizipata Wizara ya Ardhi kwa msaada ndipo walipobaini kuwa kilakitu kilikuwa kimeghushiwa.
Mkataba huo unaonyesha ulisainiwa Juni 29 mwaka 2012, ambapo siku hiyo hiyo mkataba wa mauziano ulifanyika, taarifa ya uthaminishaji na kubadili mmiliki.
“Shahidi anatajwa kuwa ni Victoris Paulo ambaye simfahamu kabisa,”alieleza mzee huyo.
Amesema mkataba unaeleza kuwa aliwahi kuridhia nyumba yake ya kuishi iuzwe kwa ridhaa yake.
“Sijawahi kufanya hivyo na pia picha yangu iliyotumika kwenye mkaba niliitumia serikali ya mtaa,”alisema.
“Mei 16 mwaka 2014 tukiwa safarini nyumbani Bukoba , ambapo Mandago alituma watu nyumbani, kupitia kampuni ya Udalali ya Majembe Auction Mart, ambapo walivunja milango na kuanza kutoa vyombo nje.
“Nyumbani tulimuacha mtoto wetu mmoja tu wa kiume wa kidato cha pili. Walivunja na kutoa kila kitu. Tuliporejea Dar esSalaam, tulielezwa kuwa Mandago alikuwa ameuza nyumba hiyo na vyombo vyote vilichukuliwa na Majembe, “alisema.
Baadae Bejumula na Mkewe, walimuendea Mandago na kuwataka wampe sh. milioni 100 hadi 300 au awape nyumba nyingine kwa sababu alipapenda mahari ilipokuwa nyumba yao ya Bahari Beach.
“Tulikwenda mahakamani kufungua kesi lakini baadaye mwanasheria aliyekuwa anatusimamia katika kesi hiyo tulibaini anashirikiana na Mandago. Hivyo alianza kupindisha kesi tukaiondoa,” alielisema.
Kwa upande wa Bi Stella ambae ni Mke wa Mzee Bejumla ,alisema kutoka kipindi hicho familia yake ilikuwa imepoteza dira ya maisha kwani hata mali zao zilizokuwa zimechuliwa na Majembe, ziliharibika kwa mvua licha ya Majembe kukiri kuzichukua ili kuzihifadhi.
“Tunaishi maisha ya taabu sana .Familia imepoteza dira. Matunda ya kazi yetu yote tuliyoitumikia serikali imekwenda bure. Tulijitahidi kujenga nyumba ya kisasa lakini sasa wanaishi watu wengine. Sisi tuliotoa jasho tunaishi maisha ya taabu,”alisema Bi Stella.
Hata hivyo wameamua kumshtakia (Kumuomba) Rais Dk. John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar esSalaam, Paul Makonda kuwasaidia kwani kwa sasa familia imeshindwa hata kufuatilia haki yao kutokana na kuishiwa fedha.
“Mtuhumiwa yuko mahabusu katika ile kesi ya utakatishaji fedha iliyoisababishia Serikali Hasara ya Shilingi Bilioni 15. Hatujui atatoka lini ili tudai haki yetu.Tunaomba serikali itutazame. Nyaraka zote tunazo na ushahidi wa kutaperiwa upo,”alieleza Stella kisha kuangua kilio cha haja kilichosababishwa kupata presha ya kushuka ghafla kuanguka chini.
No comments:
Post a Comment