Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akimfariji Bi. Stella Bejumula mstaafu alietapeliwa nyumba yake
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo
ametembelea
na kutoa pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella
Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa Nyumba yao
ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki inatendeka bila
kuvunja sheria.
RC Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa
vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi,
Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya nyumbani
baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote.
Stori ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya
kufanya kazi kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa
kuvumilia na kutokwa na machozi kutokana na namna inavyouzunisha kuona mnyonge
anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu anatokea
mtu anamdhulumu Mali yake.
Makonda amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa
kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Benki, Muuzaji wa nyumba,
Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu wa ardhi.
Kwa sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja
aliejitolea kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo
alioonyesha.
Kwa upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia
kitendo cha RC Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha
kuwatembelea na kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa
utendajikazi wa RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea
Chakula kwakuwa wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo
vyakula ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi
wanyonge.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda akikabidhi vyakula na mahitaji mbalimbaya kibinadamu alipokwenda kuwatembelea wastaafu hao waliotapeliwa nyumba
Hii ndio nyumba waliotapeliwa wastaafu hao
No comments:
Post a Comment