
Dar es salaam.
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda anaendelea kuwashughulikia Matapeli ambao wamekuwa wakikudhulumu watu mali zao, Mzee mwingine amejitokeza anaefahamika kwa Jina la Abdul Rajab Zahor mkazi wa ilala Jijini Dar es salaam amelalamika juu ya Mtu alimpangisha nyumba yake ya Ghorofa iliyopo kariakoo Mtaa wa AGREY ambayo pia ni ya urithi, kutaka kudhulumiwa na mpangaji huyo.
Mzee Abdul Rajab Akizungumza na Vyombo vya Habari.
Tukio hilo limeshuhudiliwa leo na vyombo vya Habari ,ambapo mzee huyo amedai kuwa eneo hilo waliingia Mkataba na bwana mmoja ambae amefahamika kwajina la EDWARD MOSHA Ambapo mkata huo ulikuwa ukimtaka ajenge ghorofa mbili ,huku la chini atakuwa akimiliki yeye na juu watamiliki wenye eneo husika.
Hapa ni Kariakoo mtaa wa Agray na Hili Ndilo Ghorofa analodai kutaka kudhulumiwa.
Kutoka na hayo ,Amedai kuwa hali imekwenda tofauti na makubaliano ya Mkataba na kusema kuwa Bw.Edward alijenga ghorofa hilo kinyume na matakwa ya Mkataba huo ,huku akisema mkataba ulimtaka bwana Edward kujenga maduka thelathini na mbili (32) na maduka matatu watamiliki wenye eneo husika .
"Nyumba hii naona kama nataka kudhulumiwa maana ule mkataba uliofanywa si mkataba wa halali mpaka sasa mara ya kwanza tulitia saini nikiwa na ndugu zangu ambao kwa sasa wote wakufa na nimebaki mimi peke yangu ambapo tuliweka saini mwaka 2008 na tukakaa miaka mitatu bila eneo hili kujengwa na marehemu kaka angu alimwandikia barua bwana Edward Mosha kwamba kama ameshindwa kujenga hapa basi aache tumtafute mtu mwingi ajenge, baada ya kumwambia hivyo mnamo mwaka 2012 ndo akajenga ghrofa kinyume na makubaliano huku makubaliano ni kujenga ghorofa mbili na yeye hakufanya hivyo" AMesema Mzee Abdul Rajab
Amedai kuwa ghorofa hilo amejenga vile anavyotaka yeye nakuweka maduka zaidi ya 30 na kuwapa maduka matatu ambapo baadae duka moja aliwapokonya na kusema kuwa atawarudishia ndani ya muda wa miaka miwili na hatimae kuwanyang"anya maduka yote.
"Tumevuta subira kwa muda mrefu lakini duka hilo hakuturudishia na mpaka kaka yangu amefariki hakuna chochote tulichokipata na hatimae maduka yote amechukua "Amesema Mzee ABDUL RAJAB
Aidha Mzee Abdul ameendelea kusema kuwa Bwana Edward Mosha aliamua kushirikiana na wajukuu zake kwa kuwapa pesa pasina mzee huyo kujua chochote.
"mimi ndie muhusika halali wa mkataba huu na ndugu zangu ambao wametangulia mbele ya haki na mimi ndie niliefanya mambo yote haya lakini bwana edward aliamua kushirikiana na vijana wangu (wajukuu) kuwapa pesa ili suala hili liishie juu kwa juu"Amesema Mzee abdul
Mzee Abdul amedai kuwa alimwita ili wazungumze kama atakuwa na nia ya kuinunua nyumba hiyo lakini hakuweza kukubali mwito huo na hatimae hakutaka kufanya hivyo.
"Amekuwa kila kitu anaamua yeye kama yeye ni mwenye nyumba na wakati yeye n i mpangaji na mnavyoliona jengo hili ndugu zangu ,mimi sipati hata senti tano nimekuwa mtu wa kuzungushwa tu"Amedai Mzee Abdul
Amesema mkataba huo haukwenda kama vile walivyopanga hivyo bwana Edward amekuwa mwamuzi wa mwisho kwa kila jambo alitakalo.
Kutokana na hayo yote amemwomba Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salam kuingilia kati na kumsaidia Ghorofa hilo lirudi kwenye imaya yake.
"Namwomba Mkuu wa Mkoa pamoja na serikali kwa ujumla kupitia waziri Lukuvi mwenye dhamana ya ardhi wanisaidie jambo hili maana sina pakukimbilia ,wenzangu wote wameshakufa nimebaki mimi mwenye sinauwezo wakuweza kupambana na bwana Edward (Mpangaji) nawaomba wanisaidie "Aliongea kwa Msisitizo Mzee Abdul.
No comments:
Post a Comment