Benki ya TPB yasaini mkataba wa mahusiano na
taasisi ya Tanzania skauti association lengo ikiwa ni kuweza kusaidiana
katika kuijenga Taasisi hiyo ya skauti.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshindi amesema lengo la
kusaidia kuijenga Tanzania skauti association na kusaidia kutengeneza data za
kuwatambua wanachama wao waliopo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na kutoa kadi
za kisasa kwa ajili ya wanachama wao
Amesema katika kutengeneza mahusiano yao kutawasaidia kutoa
elimu kwa Vijana namna ya kuweka akiba kwa manufaa yao na kizazi kijacho
pia.
"Niwashukuru Sana Tanzania skauti association walivyokuja
na wazo hili kwani kutasaidia kuelimisha na kutoa elimu kwa Vijana ya namna ya
kuweka akiba kwani Vijana wengi hawajui njia za kuweka akiba yao ya mbeleni.
"Alisema Mkurugenzi wa TPB
Aidha amesema wataweza kuwasaidia Tanzania skauti association
kukusanya mapato yao kwani watakuwa tayari wamefahamu wanachama wao kutokana na
ladies zitakazotolewa.
Kwa upande wake kamishna Wa chama cha skauti Tanzania Abdulkarim
Shah, meishukuru Benki ya TPB kwa kukubali kusiani mkataba wa mahusiano na kuweza
kupata kadi zitakazotambulisha wanachama,ambapo amesema itasaidi kuwatambulisha
na kufahamu wanachama wa skauti anapopatikana.
No comments:
Post a Comment